LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 30, 2020

RWANDA YAONGOZA KWA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA AFRIKA MASHARIKI


  Rwanda imethibitisha visa 10 vipya vya maambukizi ya ugonjwa wa Corona  siku ya Jumapili na kufikisha 70 jumla ya watu wanaougua corona, Wizara ya afya Rwanda imetangaza.

Katika hotuba yake kwa taifa usiku wa Ijumaa Rais Paul Kagame alisema idadi hiyo itaendelea kuongezeka kwasababu wale waliotangamana na waathirika wanaendelea kutafutwa.

Katika visa vya hivi punde vya maambukizi, watu sita walitokea Dubai, wawili kutoka Afrika Kusini, mmoja kutoka Nigeria na mwigine alikuwa amesafiri maeneo ya Afrika mashariki hivi karibunii, ilisema taarifa ya wizara ya afya nchini humo.

Rwanda inaongoza kwa visa vya maambukizi ya ugonjwa wa corona katika kanda ya Afrika Mashariki ikiiwa na wagonjwa 70, ikifuatiwa na Kenya 42, Uganda 33, Tanzania 19, huku Burundi na Sudan Kusini zikiwa hazijarekodi visa vyovyote vya maambukizi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages