Meneja Mwandamizi wa NMB Kitengo cha Biashara za Serikali - Adelard Mang'ombo akimkabidhi msaada wa vifaa vya afya, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sofia Mjema ambavyo ni vitanda vitano pamoja na mashuka katika Kituo cha Afya Pugu Kajungeni vyote vyenye thamani ya shilingi milioni 5.
Mkoani Kilimanjaro,
NMB kupitia Meneja wa Kanda ya Kaskazini, Aikansia Muro, alikabidhi msaada wa
vitanda vitano vya kulalia, viwili vya kujifungulia akina mama, mashuka 25,
magodoro 5, pamoja na hundi ya Sh. Milioni 16 kwa ajili ya wakulima wa zao la
vanilla Mkoani humo
BENKI ya NMB imekabidhi
misaada mbalimbali ya vifaa tiba na vifaa vya elimu katika Mikoa ya Dar es
Salaam na Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa kurejesha kwa jamii
asilimia moja ya faida yao kupitia Programu ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).
Jijini Dar es
Salaam, NMB imetoa msaada yenye thamani ya Sh. Mil. 15 kwa Shule ya Sekondari
Tambaza, iliyopo Upanga na Kituo cha Afya Pugu Kajiungeni wilayani Ilala jijini
Dar es Salaam, wakati Mkoani Kilimanjaro imekabidhi vifaa tiba kwa Hospitali ya
Wilaya ya Hai.
Tambaza Sekondari,
imepokea msaada wa vitanda 80 vya kulalia wasichana wa shule hiyo vyenye
thamani ya Sh. Mil. 10, vilivyokabidhiwa na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es
Salaam, Badru Idd na kupokelewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano na Mazingira), Mussa Zungu.
Katika hafla ya
kukabidhi vifaa tiba katika Kituo cha Afya Pugu Kajiungeni, NMB ilikabidhi
msaada huo wenye thamani ya Sh. Mil. 5 kupitia kwa Meneja Mwandamizi wa NMB Kitengo
cha Biashara za Serikali, Adelard Mangombo, na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya
Ilala (DC), Sofia Mjema.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇