MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu (kushoto) akikabidhi mifuko ya saruji msaada kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Jengo la Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Singida.
MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturuakizungumza na baadhi ya viongozi wa CCM , alipokuwa akikagua ujenzi wa jengo hilo la Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Singida.
Na Sakina abdulmasoud
MBUNGE
wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amekabidhi mifuko 30 ya saruji
ikiwa ni namna ya kuunga mkono ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Umoja wa
Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM)Mkoawa Singida.
Ujenzi huo ni mpango wa jumuiya hiyo wa kuhakikisha wanajenga nyumba za watendaji wao kwa kila mkoa nchi nzima.
Akikabidhi
mchango huo machi 28 Mtaturu amewapongeza UVCCM chini ya Mwenyekiti
wake Kheri James kwak uja na mpango huo wenye lengo la kuwapa makazi ya
kudumu watendaji wake.
“Mpango
huu ni mzuri sana,niwapongeze UVCCM na viongozi wenu kwa kuweka
mikakati inayoacha alama,nimekabidhi mifuko hii ya saruji 30 lakini pia
ninachangia pesa ya kuwalipa mafundi sh 80,000 na ninawaahidi kuendelea
kuwaunga mkono katika jambo hili jema mnalolifanya,”alisema Mtaturu.
Amewapongeza
UVCCM mkoa wa Singida chini ya mwenyekiti wake Dkt Denis Nyiraha kwa
kuweka Mpango wa Utekelezaji wa maazimio ya Taifa ambapo kwa sasa wapo
mbioni kumaliza nyumba ya Katibu wa Mkoa ili hatimaye waendelee
kusimamia kwa ngazi za Wilaya.
“Hii
ndio tofauti ya CCM na vyama vingine vya mfukoni ambavyo hata Ofisi
havina,hivyo hawawezi kuwa na Mpango huu ambao unafanywa tu na Jumuiya
ya vijana ya CCM,”aliongeza Mtaturu.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Dkt Nyiraha amemshukuru mbunge
Mtaturu kwa utayari wake wa kuunga mkono mpango wa Ujenzi wa nyumba ya
mtendaji wa Uvccm Mkoa.
“Kwa
niaba ya jumuiya hii mkoa nitoe shukrani zetu kwako,tunatambua siku
zote kila tunavyokufikia kwa mambo mbalimbali yanayohusu Jumuiya yetu
umekuwa mwepesi sana,”alisema.
Katibu
wa UVCCM Mkoa George Silindu amesema hiyo ni heshima kubwa kwa
watendaji kupatiwa makazi yenye heshima yatakayoleta utulivu na kuongeza
ari ya kazi.
“Matarajio
yetu hadi kufikia mei,2020 nyumba hii iwe imekamilika ili Mkoa ushuke
kusimamia ujenzi ngazi ya wilaya ambao utagharimu sh milioni 25 kwa
nyumba moja,”alisema Silindu.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment
ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇