Spika wa Bunge, Job Ndugai (Mb), akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mabadiliko ambayo yatafanyika katika Utaratibu wa Uendeshaji wa Shughuli za Bunge wakati wa Mkutano wa Bunge wa Bajeti unaotarajiwa kuanza kesho Jijini Dodoma. Spika ametangaza mabadiliko kadhaa ambayo yatafanyika wakati wa uendeshaji wa shughuli za Bunge ili kukabiliana na janga la Ugojwa wa Korona. Wakwanza kulia ni Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson.
Spika wa Bunge Job Ndugai (katikati) akizungumza wakati wa Kikao cha kamati ya Uongozi ambayo ilikutana ili kujadili na kupitisha shughuli zitakazofanyika wakati Bunge la Bajeti linalotarajiwa kuanza kesho Jijini Dodoma. kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson na Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama.
Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson akizungumza wakati wa Kikao cha kamati ya Uongozi ambayo ilikutana ili kujadili na kupitisha shughuli zitakazofanyika wakati wa Bunge la Bajeti linalotarajiwa kuanza kesho Jijini Dodoma. Katikati ni Spika wa Bunge Job Ndugai na Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mhe. Jenista Mhagama.
Wajumbe wa kamati ya Uongozi katika kikao cha Kamati kilichokutana ili kujadili na kupitisha shughuli zitakazofanyika wakati wa Bunge la Bajeti linalotarajiwa kuanza kesho Jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇