Manispaa ya Ubungo imeanza kutoa huduma za kitabibu katika vituo vya Afya vilivyopo katika Manispaa hiyo kwa kuanza kutoa huduma hiyo katika kituo cha Afya cha Mbezi Louis
Huduma hiyo ambayo ilianza wiki hii, Machi 2, 2020 itakuwa ya wiki tatu na wiki ya pili huduma zitahamia kituo cha Afya Kimara na wiki ya tatu itamalizia katika kituo cha Afya Makurumla.
Huduma zitakuwa zikitolewa bure katika wiki zote tatu ambapo Madaktari watakaokuwa wakitoa huduma katika vituo hivyo ni madaktari bingwa wa magonjwa ya watoto, madaktari bingwa wa magonjwa ya kinamama na wataalam wa upasuaji.
Wananchi wote waliopo Manispaa ya Ubungo wanahimizwa kijitokeza kwa wingi ili waweze kupata huduma hii kutoka kwa madaktari hawa bingwa.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
MANISPAA YA UBUNGO
Your Ad Spot
Mar 4, 2020
MADAKTARI BINGWA WAANZA KUTOA HUDUMA KATIKA VITUO VYA AFYA MANISPAA YA UBUNGO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇