Halmashauri ya Jiji la Tanga imeendelea kutoa tahadhari kwa wakazi wa jiji hilo kutokana mlipuko wa Ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na kirusi cha Corona kwamba wananchi waweze kusimamia maagizo muhimu yanayotolewa na serikali ikiwemo mikusanyiko isiyo ya lazima.
Hayo aliyasema Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Selebosi wakati akizungumza katika baraza la madiwini lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo ambapo alisema wapo watu bado wana mizaha na janga hilo ugonjwa wa Cona kwani wanalichukulia utani jambo ambalo ni chukizo hata Mwenyenzi Mungu.
Alisema wapo watu wanaendelea kufanya mikusanyiko yasiyo ya lazima ambayo hayatakiwa kutokana maelekezo yaliyotolewa na serikali didhi ya tahadhari ya ugonjwa huo, wakiwemo baadhi ya wanafunzi wanaendelea michezo ya mipira kwenye viwanja vya nyumbani bila kujua madhara ya mikusanyiko hiyo.
“Jukuma la kuwaelimisha watu hawa pamoja na wanafunzi hao ni sisi wawakilishi wa wananchi kupitia mabaraza yetu ya kata ili kuweza kuzuia mlipuko wa ugonjwa huo kwani kama hatutakuwa makini ni vigumu kuepuka janga hilo” alisema Mstahiki Meya.
Kwa upande wakw mkuu wa Wilaya ya Tanga Tobias Mwilapwa aliwapongeza watendaji wa halmashauri kwa kuonyesha juhudi za kuonyesha tahadhari didhi ya ugonjwa huo kwani wameka ndoo za maji tiririka wenye ofisi zote za Halmashauri kwa ajili ya kunawia mikono jambo ni utekelezaji wa agizo la serikali .
Aidha alisema wanachopaswa kufanya ni kuendelea na ushirikiano wa dhati katika ngazi zote kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi wote wa jiji hilo ili waendelee kuchukua tahdhari na kujua umuhimu wa kuchukua tahadhari hiyo bila kuwa na mizaha.
Awali akizungumza katika baraza hilo Diwani wa kata ya Msambweni Abdulrahman Hassan alitoa ushauri wa mwenyekiti wa kikao hicho cha baraza ambacho ni kawaida kikanuni,Mstahiki Meya wa jiji kwamba wakati mwingine inapotokea suala la kutoa elimu kwa wananchi hususan juu ya janga kama la Corana inapaswa wao kama wawakilishi wa wananchi kupata taarifa ili wapeleke elimu hiyo kwa wananchi wao.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇