LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 26, 2020

DRC YATANGAZA HALI YA HARI KUHUSU CORONA


Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza hali ya dharura na kuufunga mji mkuu wa Kinshasa kujitenga katika hatua ya kupambana naa maambukizi ya virusi vya Corona.

Rais Félix Tshisekedi alitangaza kuchukua hatua hizo jana jioni kupitia televisheni ya taifa.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema kuwa, pamoja na kufunga mipaka ya nchi, kusitisha safari za ndani na nje ya mji mkuu zikiwemo za mabasi, ndege na majini, utekelezaji wa haraka unahitajika.

Mpaka sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeripotiwa kuwa na wagonjwa 48 wa covid-19 na watu watatu kufariki dunia kutokana na maambukizi ya ugonjwa huo.

Mji mkubwa wa pili wa taifa hilo, Lubumbashi, ulifungwa kwa saa 48-siku ya Jumatatu baada ya watu wawili kutambuliwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Mmoja alikuwa mwanamume mwenye miaka 47 na mtoto wake wa kiume wa miaka 13, walikuwa wametokea mji mkuu wa Kinshasa siku ya Jumapili.
 

1 comment:

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages