LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 17, 2020

CCM YASITISHA MIKUTANO KUKABILIANA NA CORONA NA YAMTAHADHRISHA MBOWE

Katibu wa Halmashauri Kuu ya taifa (NEC) ya CCM, Idara ya Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akizungumza na waandishi wa habari, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam, leo.










LUMUMBA St. Dar es Salaam
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesitisha shughuli zote zinazohusu mikusanyiko ya watu wengi, ikiwa ni hatua za kuunga mkono serikali katika kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona 

Hatua hiyo imetangazwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Idara ya Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Amesema, mikutano yote ikiwemo ya ndani na ya hadhara yenye asili ya mikusanyiko ya watu wengi, itasimama hadi pale chama kitakapotoa maagizo mengine.


“CCM taasisi kubwa, inazo shughuli zake zinazoendelea kutoka mwanzo hadi mwisho wa mwaka, matukio makubwa ya ujenzi wa chama ya nje na ndani ya jamii.

Maelekezo shughuli zote za CCM zenye asili ya mikusanyiko mikubwa, iwe ya ndani au ya hadhara. Shughuli hizo zisitishwe mara moja kuanzia leo,” amesema Polepole.

Polepole amesema ziara za viongozi wa CCM zilizokua zimeanza au zinazoratarajiwa kufanyika zitasimama kuanzia leo, hadi pale hali itakapokua shwari.

Aidha, Polepole amekosoa uamuzi wa Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alioutoa jana tarehe 16 Machi 2020, kwamba wataanza mikutano ya hadhara Aprili mwaka huu.

“ Freeman Mbowe anahamasisha watu kufanya mikutano ya hadhara hapa Watanzania mpime nani anawapenda, nani anataka kuwatumia.

Corona inauwa kweli na ukiipata ni rahisi kuambukiza wengine na eneo rahisi kuambukizana ni kwenye mikusanyikon,”  Amesema  Polepole.

Ugonjwa huo ulioanzia katika mji wa Wuhan, China Desemba, 2019 na baadaye kuanza kusambaa nchi mbalimbali umesababisha vifo vya watu zaidi ya 4,500 huku Tanzania ikiwa nchi ya tatu Afrika Mashariki kuwa na mgonjwa wa corona baada ya Kenya na Rwanda.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages