LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 3, 2020

WANAJESHI KUMI WA JWTZ WAFARIKI DUNIA WAKATI WAKIFANYA MAZOEZI

DAR ES SALAAM, Tanzania
Wanajeshi kumi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wamefariki dunia kwa kinachohofiwa kuwa walikula chakula chenye sumu walichonunua njiani wakati wakitembea wakiwa katika mazoezi ya kawaida katika eneo la Msaata, Chalinze mkoa wa Pwani.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (pichani), amesema kuwa sampuli za wanajeshi hao waliopoteza maisha katika mazoezi ya kijeshi zimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali  kwa ajili ya uchunguzi.

"Tunahisi walikula chakula chenye sumu, labda wakati wanatembea walinunua vyakula barabarani vikawadhuru. Mazoezi yalikuwa ya kawaida tu. Tumepeleka sampuli za waliofariki kwa Mkemia Mkuu ili kubaini chanzo hasa cha vifo," alisema Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo akizungumzia vifo hivyo vilivyotokea Januari 30, 2020.

Mabeyo ameyasema hayo leo, Ikulu ya Dar es Salaam, kwenye hafla ya Rais Dk. John Magufuli kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni. 

Kwa mujibu wa Mabeyo, wanajeshi hao walikuwa kwenye mazoezi ya kawaida ya kutembea na kwamba baada ya saa mbili hali zao zilianza  kubadilika wakiwa eneo la Msata ikabidi wapelekwe hospitali kuu ya Jeshi ya Lugalo.

Jenerali Mabeyo amesema baada ya kulazwa hospitalini hapo, baadhi yao walifariki dunia na wengine hali zao ziliimarika na kwamba hadi sasa kuna majeruhi watano.

Awali akizungumza kwenye hafla hiyo, Rais Magufuli alitoa pole kutokana na vifo vya watu 20 katika kongamano la Mhubiri wa Kikristo, Boniface Mwamposa vilivyotokea mjini Moshi, vifo vya watu 21 mkoani Lindi baada ya nyumba zao kusombwa na maji na vifo vya wanajeshi hao kumi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages