LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 4, 2020

WADAU WATAKA TOLEO JIPYA LA MAPITIO YA SHERIA MBALIMBALI

Jaji  wa Mahakama Kuu, George Masaju akibadilishana mawazo na  Mawakili wa   Serikali , Tunu Temu na Anna Mkongwa, Wakati  Mhe. Masaju alipotembelea banda la  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Viwanja vya Nyerere Square  Jiji Dododma, ambako wiki  ya utoaji elimu  kuhusu masuala ya kisheria . Pamoja na mambo mengine Mhe. Masaju alipongeza Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kufungua Ofisi  katika Mikao  Nane na akashauri  Ofisi hizi zienee  Mikoa yote kutoka na mahitaji makubwa ya huduma za Ofisi ya Mwanasheria Mkuu. 








Na Mwandishi wetu,Nyerere Square, Dodoma

Wadau mbalimbali wakiwamo, Majaji, Wanasheria na Wananchi wa kawaida, wameiomba Ofisi ya  Mwanasheria Mkuu wa Serikali kufanya kila liwezakanalo kuhakikisha kwamba, kunachapishwa  toleo jipya la mapitio ya sheria mbalimbali.

Kwa mujibu wa wadau hao,  tolea la mwisho lilichapishwa mwaka 2002 na hakujawa na chapisho  jipya, jambo linalowapatia ugumu mkubwa wa rejea wakati wa utoaji wa maamuzi mbalimbali.

Maoni na mapendekezo ya wadau hao, ni kuitaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhakikisha kwamba, jitihada zinafanyika za kuwa na toleo jipya ili pamoja na mambo mengine  kuondoa hatari ya kutoa uamuzi au ushauri kwa kutumia sheria ambayo tayari imekwisha kufanyiwa marekebisho au imefutwa kabisa.

Zaidi ya  wadau  kumi ambao wamefika katika Banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali lilipo  katika Viwanja vya Nyerere Square, wameelezea shida na mkanganyiko wanaoupata wakati wa utekelezaji wa majukumu yao na muda wanaopoteza kufanya marejeo ya sheria ambazo zimeshafanyiwa maboresho lakini hazipo katika  mpangilio unaoeleweka.

Wakati huo huo  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imepongezwa kwa kufungua Ofisi zake katika Mikoa kadhaa   ili kurahisha upatikanaji wa huduma za kisheria.

Pongezi hizo zimetolewa na Mhe.Jaji George Masaju wakati alipofika katika banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali lilipo katika viwanja ya Nyerere Square.

"Niwapongeze  kwa hatua hii nzuri ya kuanza kufungua Ofisi mikoani kwa sababu ni muhimu sana kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ikawa katika kila Mkoa na ikiwezekana kila  katika Halmashauri za Wilaya ili kurahisisha upatikanaji wa huduma" Akasema Jaji Masaju.

Akasema kuwa, kufisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali hadi ngazi ya wilaya inawezekana ingawa ni  kazi nzito kutokana na  uhaba wa Bajeti lakini  linawezekana ikiwa  Halmashauri zitashirikishwa ili ziingize katika mipango yao ya Bajeti kwa sababu wanahitaji huduma ya  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kwa sasa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ipo katika Mikoa ya Arusha, Tanga, Tabora, Mtwara, Kagera,  Kilimanjaro, Mwanza, na Mbeya

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages