UBUNGO, Dar es Salaam
Halmashauri ya Manipaa ya Ubungo Dar es Salaam, imetangaza kuwa Wananchi wa majimbo ya Kibamba na Ubungo katika Manispaa hiyo, kuwa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga kura limeanza tangu tarehe 14/02/2020 na litafanyika kwa muda wa siku saba kuanzia tarehe hiyo hadi tarehe 20/02/2020 litakapomalizika.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Uandikishaji katika Majibo hayo na kusambazwa na Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa hiyo ya Ubungo Beatrice Dominc, wanaohusika katika zoezi hilo ni wananchi wote waliotimiza umri wa miaka 18 na wengine wote wenye sifa lakini hawakujiandikisha mwaka 2015.
Taarifa hiyo imesema, zoezi litahusisha kutoa kadi mpya kwa wapi gakura ambao kadi zao zimepotea au kuharibika, kuhamisha taarifa za wapiga kura waliohama kata au majimbo yao na kwenda kwenye maeneo mengine ya kiuchaguzi, Kurekebisha taarifa za wapigakura ambazo zilikosewa kama majina, kuondoa taarifa za wapigakura walisokuwa na sifa ikiwemo kufariki dunia.
Pia wale wenye vitambulisho vya mpigakura hawana haja ya kwenda kituoni mpaka wakati wa kukagua orodha ya wapigakura itakayobandikwa vituoni mwisho mwa zoezi kukamilika na vituo vitakuwa wazi kuanzia saa 2.00 asubuhi na kufungwa saa 12.00 jioni kwenye mitaa na kata zote katika Manispaa ya Ubungo
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇