Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
WAZIRI wa Madini Dotto Biteko amesema kuwa cheti cha kuuza na kusafirisha madini ya bati nje ya nchi kitatolewa kesho na kueleza kuwa cheti hicho ni hatua kubwa kwa wachimbaji wa madini nchini katika kukuza na kuimarisha sekta hiyo muhimu.
Akizungumza na wawekezaji katika sekta ya madini katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Mwalimu Nyerere (JNICC) leo jijini Dar es Salaam Biteko amesema Serikali ipo pamoja na wachimbaji hao hasa kwa kushirikiana nao ili kuendeleza sekta hiyo adhimu.
"Mkutano huu ni wa kutangaza fursa na kubwa zaidi ni kesho ambapo tutapokea cheti cha kusafirisha madini ya bati nje ya nchi kibali ambacho hatukuwa nacho awali" ameeleza Biteko.
Pia amesema mafanikio katika sekta hiyo ni makubwa na yenye tija kwa taifa kwani hata ukusanyaji mapato kwa sasa mapato yanayokusanywa yamefikia zaidi ya shilingi bilioni 300.
Awali akizungumza wakati wa warsha hiyo Mwenyekiti wa Shirikisho la wachimbaji wadogo wa madini Tanzania (FEMATA) John Bina ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya madini kwa kuonesha ushirikiano hasa katika utatuzi wa changamoto.
" Changamoto zilizokuwa zinatukabili zimetatuliwa kwa asilimia 80 na tunafurahi kwa sasa Sheria ya madini ni faaafu na Tanzania ni sehemu salama ya uwekezaji" Ameeleza Bina
Aidha amewataka wachimbaji hao kushirikiana katika kuendeleza sekta hiyo na kueleza kuwa ikitokea kukawa na siku ya madini, wachimbaji wamependekeza siku hiyo iitwe "Magufuli Minerals Day" na hiyo ni kutokana na mchango mkubwa wa Rais Magufuli katika kuinua na kuweka mazingira bora kwa ukuaji wa sekta hiyo.
Mkutano huo wa Kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya madini nchini kwa mwaka 2020 uliobeba kauli mbiu ya "Uwekezaji na Ushiriki katika sekta ya madini" umehudhuriwa na mawaziri wa madini kutoka nchi mbalimbali Afrika ikiwemo Uganda na Congo na utafungwa kesho na waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Waziri wa Madini Mh. Dotto Biteko akifungua mkutano wa kimataifa wa uwekezaji kwenye Sekta ya Madini unaoendelea jijini Dar es Salaam tarehe 22 Februari, 2020 ambao unakutanisha wadau wa madini kutoka ndani na nje ya nchi.
Naibu Waziri wa Madini Mh. Stanslaus Nyongo akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa uwekezaji kwenye Sekta ya Madini unaoendelea jijini Dar es Salaam tarehe 22 Februari, 2020 ambao unakutanisha wadau wa madini kutoka ndani na nje ya nchi.
Waziri wa Madini wa Uganda Bi.Sara Nkoniakizungumza katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila mkutano wa kimataifa wa uwekezaji kwenye Sekta ya Madini unaoendelea jijini Dar es Salaam tarehe 22 Februari, 2020 ambao unakutanisha wadau wa madini kutoka ndani na nje ya nchi.
Kamishna wa Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma akielezea fursa zilizopo kwenye Sekta ya Madini Tanzania katika mkutano wa kimataifa wa uwekezaji kwenye Sekta ya Madini unaoendelea jijini Dar es Salaam tarehe 22 Februari, 2020 ambao unakutanisha wadau wa madini kutoka ndani na nje ya nchi.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifurahia hotuba ya Waziri wa Madini Mh. Dotto Biteko wakati alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa uwekezaji kwenye Sekta ya Madini unaoendelea jijini Dar es Salaam tarehe 22 Februari, 2020 ambao unakutanisha wadau wa madini kutoka ndani na nje ya nchi.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (katikati) akifuatilia mada mbalimbali zinazowasilishwa kwenye mkutano wa kimataifa wa uwekezaji kwenye Sekta ya Madini unaoendelea jijini Dar es Salaam tarehe 22 Februari, 2020 ambao unakutanisha wadau wa madini kutoka ndani na nje ya nchi.
Washiriki mbalimbali wakiwa katika mkutano huo.
Waziri wa Madini Mh. Dotto Biteko akiwa meza kuu pamoja na waziri wa Madini wa Uganda Bi.Sara Nkoni pamoja na mawaziri na viongozi mbalimbali wanaoshughulikia madini
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada wakati zikiwasilishwa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇