Mkuu huyo wa TAKUKURU ameendelea kueleza kuwa mlalamikaji alifika ofisini kwao na kutoa malalamiko ambapo walianza kazi ya uchunguzi na mtuhumiwa alikiri kuwa alichukua fedha hizo kwa madai kuwa alikuwa akimkopesha mwalimu kwa muda mrefu na riba ikaongezeka
“Hata hivyo riba yenyewe haikuwa na viwango vya kueleweka hivyo mtuhumiwa amerudisha fedha taslimu shilingi milioni 24; na ameahidi kumalizia milioni tano baada ya mwezi mmoja” alisema Nakua
Kwa upande wake Mwalimu Ngairo amesema alikuwa akikopa fedha kidogo kidogo kutoka kwa mfanyabiashara huyo hadi deni lake likafikia shilingi milioni 16.4;
“Siku ya tukio alinifuata nyumbani na kuniambia mafao yako yametoka twende ukachukue fedha unilipe deni langu” alisema Ngairo
Ameendelea kueleza kuwa mara baada ya kutoa kiinua mgongo chake cha shilingi milioni 49 mtuhumiwa alimnyang’anya begi zima na kumpa milioni tatu tu
Kufuatia tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera ametaka wafanyabiashara wanaokopesha kwa riba kufuata taratibu za kifedha zilizowekwa
“Hawa wamezidi sasa hapa mkoani wamekuwa wakipora fedha za watu kwa madai ya riba kuongezeka, serikali hii haitavumilia wanyonge kunyanyaswa” alisema Homera
Aidha mkuu huyo wa mkoa wa Katavi ameisifu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutetea wanyonge
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇