LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 10, 2020

SUMAYE AREJEA CCM LEO, APOKEWA NA DK. BASHIRU, OFISI NDOGO YA MAKAO MAKUU YA CCM, LUMUMBA, JIJINI DAR ES SALAAM

<<Waziri Mkuu wa zamani Frederick Sumaye akiwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ally baada kuingia nae ukumbini kwenye Kikao Maalum cha Baraza la Wadhamni wa Chama Cha Mapinduzi, kinachofanyika leo katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Pichani, Sumaye akizungumza wakati akitangaza kurejea CCM. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa CCM, Anna Abdallah





Lumumba, Dar es Salaam
Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye leo ametinga Ofisdi Ndogo ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Lumumba jijini Dar es Salaam, na kutangaza kurejea tena CCM.

Sumaye ambaye wakati wa vuguvugu la Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 alikihama Chama Cha Mapinduzi na kujiunga na Chama cha upinzania cha Chadema, ametangaza kurejea CCM  akiwa na Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally kwenye Kikao Maalum cha Baraza la Wadhamnini wa CCM.

Mapema Desemba 4, 2019 Sumaye alitangaza kuondoka Chadema na akisema anapumzika kufanya shughuli za siasa na kwamba atabaki kuwa mshauri kwa Chama chochote cha siasa kitakacho hitaji ushauri wake.

Akizungumza wakati huo, Sumaye alisema kwamba alikosea kujiunga na Chadema akisema kwamba alikwenda huko akidhani kuwa ndiko kuna Demokrasia zaidi kumbe sivyo.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages