LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 18, 2020

SOKO TEGETA LATEKETEA KWA MOTO

  Moto ambao chanzo chake hakijajulikana umeteketeza vibanda saba katika soko la Tegeta Nyuki Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Kinondoni, Musa Taibu amesema moto huo ulianza saa 6 usiku.

“Ni kweli moto umeshika sehemu ya maduka na sio soko lote, vibanda saba vimeteketea. Baada ya kupata taarifa polisi kwa kushurikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji walifanikiwa kuuzima,” amesema.

Kamanda Taibu amesema uchunguzi umeanza kubaini chanzo na hasara iliyosababishwa na moto huo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages