LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 6, 2020

POLEPOLE AFUNGUKA KUHUSU MJADALA UNAOENDELEA KUHUSU MARIDHIANO

KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekuwa kikifuatilia mijadala na mapendekezo yaliyotolewa na vyama vya Upinzani kuhusu kufanya maridhiano na kusema kuwa vyama vya upinzani vimeshashindwa tangu mwanzo kuzingatia hatua za msingi kabla ya kufikia hatua ya maridhiano hivyo kukosa uhalali wa kutaka maridhiano.

Polepole amesema hayo leo wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, katika Mkutano wa kuadhimisha miaka 43 ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi ambapo alisema kimsingi maridhiano huanza kwa kuwa na uelewa wa pamoja katika mambo ya msingi, pili kujenga muafaka na tatu kuwa  na maridhiano yenyewe.

Akifafanua kuhusu dhana na nadharia ya maridhiano, Polepole amesema, kwanza kuwepo na uelewa wa pamoja juu nini watanzania wanataka, kazi kubwa ya maendeleo ambayo imekwisha kufanyika nchini na kubadilisha kabisa hali na ustawi wa watu, pili ni kuwa muafaka wa kitaifa kwa maana ya kukubaliana katika kazi nzuri ambayo imefanyika na katika yale ambayo hakuna muafaka ndio tunakwenda katika maridhiano.

Awali akihutubia mkutano huo wa maadhimisho ya miaka 43 ya CCM, Ndg Polepole ameeleza ni kwa namna gani Chama cha Mapinduzi kimejipanga kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020, huku akiangazia mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka 43 ya CCM na kwa umahsusi mafanikio ya serikali ya awamu tano chini ya Ndg. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM.

Kauli mbiu ya Miaka 43 ya CCM ni Tuliahidi, Tumetekeleza na Tunaahidi Tena kuchapa kazi kwa juhudi, Ubunifu na Maarifa Zaidi

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages