Na, Geofrey A. Kazaula
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Josephat Kandege ameelezea kuridhishwa kwake na miradi ya
barabara iliyotekelezwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini
Tarura katika Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.
Aliyasema hayo wakati wa Ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya
maendeleo Mkoani Mwanza ambapo ameeleza kuwa mafanikio yanayopatikana
katika Manispaa hiyo hasa katika miradi ya barabara yanatokana na
ushirikiano mkubwa uliopo kati ya wataalam wa TARURA na watumishi
wengine wa Manispaa kwa kufanya kazi pamoja na kuwaletea maendeleo
wananchi.
‘‘ Wote tumeshuhudia barabara hizi zilivyo kwenye kiwango, mafanikio
haya yanatokana na Umoja uliopo kwa watumishi wote wa Manispaa ya
Ilemela pamoja na watumishi wa TARURA kwani wanafanya kazi kwa pamoja
ili kuwaletea wananchi wetu maendeleo, kiujumla wanafanya
vizuri’’Kandege.
Aidha amesisitiza kuwa miundombinu ya barabara inapokamilika ilindwe
kwa nguvu zote na amewaagiza viongozi husika huhakikisha barabara hizo
zinafanyiwa usafi mara kwa mara na kulinda miundombinu ya barabara hizo.
Naye Meneja wa TARURA Manispaa ya Ilemela Mhandisi Clement Kihinga
amesema kuwa barabara hizo zilizotekelezwa chini ya mradi wa Tanzania
Strategic Cities Project (TSP) zimekuwa na mafanikio makubwa ikiwemo
kuinua uchumi wa wananchi na kuboresha kiwango cha maisha ya wananchi.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanailinda miundmbinu ya
barabara ilizidumu na ziendelee kuboresha maisha yao na kurahisisha
suala la usafiri na usafirishaji katika Manispaa ya Ilemela.
‘‘Serikali inatumia gharama kubwa sana kujenga barabara hizi hivyo
nitoe wito kwa wananchi kuhakikisha kila mmoja wetu anashiriki kulinda
miundombinu hii ya barabara ’’ amesema Mtaalam huyo.
Mmoja wa wananchi wa Kiseke A Ilemela Issa Shabani alisema awali
usafiri ulikuwa changamoto sana Katika barabar yao kwani miundombinu
ilikuwa mibovu sana ila baada ya baraba ya kiseke Busweru kukamilika
maisha yamepanda kiuchumi
“Sasa nafanya biashara yangu ya matunda hapa Busweru, nayabeba salama
na hayaharibiki kwani barabara ni nzuri na hata kipato changu
kimeongezeka hivyo naishukuru sana Serikali kwa kujenga barabara
hii”Alisema Shabani.
Ziara ya Kandege inaendelea Mkoani Mwanza ambapo miradi mbalibali ya
maendeleo zikiwemo barabara zinazosimamiwa na Wakala wa Barabara za
Vijijini na Mijini TARURA inatarajiwa kukaguliwa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇