Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Reli Tanzania TRC, Masanja Kadogosa amesema kuwa katika maeneo ambayo yameharibiwa na mvua Kilosa (Mororgoro), Gulwe (Mpwapwa),Igandu, Zuzu na Makutupora (Singida).
“Takribani maeneo 26 yameathirika kati ya hayo 10 yako katika hali mbaya ambapo tuta la reli na baadhi ya makalavati yamezolewa na maji”. Amesema Kadogosa.
Aidha Kadogosa amesema kuwa kutokana na hali hiyo wahandisi wa TRC wako katika maeneo mbalimbali yaliyoharibika kufanya tathimini halisi ya gharama za miundombinu ya reli iliyoathirika matengenezo ya muda mfupi yanayoendelea katika maeneo ambayo maji yanapungua ili kurejesha huduma za usafiri wa treni za abiria na mizigo ambapo hadi sasa maeneo ya kati ya Dodoma na Makutupora yamerekebishwa.
Uharibifu huo umesababisha kusimama kwa huduma ya usafiri kwa njia ya reli inayotoka Dar es Salaam hadi Kigoma, Mwanza na Mpanda mpaka ukarabati utakapokamilika.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇