LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 3, 2020

MIILI YA WALIOKUFA KWENYE KONGAMANO LA MWAMPOSA KUZIKWA LEO

   Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, amesema miili ya watu 20 waliofariki kwenye kongamano la Mtume na Nabii Mwamposa, itaagwa leo Februari 3, 2020, kwenye viwanja vya Majengo mjini Moshi.  Amesema hadi sasa tayari miili 16 imeshatambuliwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini , IGP Simon Sirro amewataka Watanzania kuwa  makini kwani kinyume na hapo itakuwa shida sana na kuongeza iko haja kamati za ulinzi na usalama za wilaya na mkoa kuanza kuyafuatilia makanisa yote nchini na hasa makanisa madogo madogo ambayo sasa yamekuwepo kila mahali.

"Sio kila padri, mchungaji basi anataka kuwachunga kondoo wake waende kuuona ufalme wa Mungu, wengine wanahangaika na utafutaji tu wa maisha. Sio kwamba nahukumu lakini kuna mambo ya kujifunza,"amesema

Kuhusu Polisi iwapo walikuwepo kwenye kongamano hilo la Mwamposa, IGP Sirro amesema ameshatoa maagizo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimajaro kufuatilia na iwapo walikuwepo polisi lazima waulizwe imekuaje hadi watu wakapoteza maisha na wao wakiwepo, kwani sheria lazima ichukue mkondo wake. 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages