LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 22, 2020

KATIBU WA UENEZI MKOA WA NJOMBE, NGOLE AWAPIGA MSASA MAKATIBU WENEZI WA KATA 16


 KATIBU wa Siasa, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe, Erasto Ngole maarufu kwa jina la Shikamoo Parachichi,  akisisitiza jambo wakati wa kikao na baadhi ya  Makatibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi wa Kata pamoja na makatibu Kata wa chama hicho kutoka Kata 16 za Wilaya ya Njombe, kuhusu wajibu wao na mikakati mbalimbali ya kuimarisha uhai wa chama katika Kata zao. Ngole amefanya vikao kama hicho katika wilaya ya Wanging'ombe. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA)
 Ngole ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kikao hicho,akiwataka viongozi hao ambao ndiyo injini ya kukisemea chama kwenda kufanya vikao na viongozi wa matawi na mashina  pamoja na kuwa karibu na wananchi kwa lengo la kutatua kero zao. Amewataka viongozi hao kuwa mstari wa mbele kukisemea chama kwa mazuri yanayofanywa  na serikali kuwaletea maendeleo wananchi. kUTOKA Kushoto ni Mwenyekiti wa Senet (Vyuo na Vyuo Vikuu) Seleman Matimbwi na Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Njombe, Kasmil Ngogo pamoja na Katibu Mwenezi Wilaya ya Njombe, Hitler Msolla.

 Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi wa CCM, Wilaya ya Njombe, Hitler Msolla akizungumza  maneno ya utangulizi katika Kikao hicho kilichoendeshwa Katibu Mwenezi wa Mkoa wa Njombe, Erasto Ngole (wa pili kushoto) wakati wa kikao hicho. Kulia ni Kaimu Katibu wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Wilaya ya Njombe, Apia Kalinga na Katibu wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Njombe, Amos Kasakula.
Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Njombe, Amos Kusakula akizungumza katika katika kikao hicho ambapo alisisitiza suala la kuwashirikisha vijana katika masuala mbalimbali katika kata zao.

 Mjumbe wa CCM  ngazi ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Njombe, Agustino Aloye akijitambulisha wakati wa kikao hicho ambacho mgeni rasmi alikuwa Katibu Mwenezi wa Mkoa huo, Ngole.
 Baadhi ya viongozi ngazi ya Kata wakiwasikiliza kwa makini wakati Ngole akiwapo somo kuhusu majukumu yao 
 Ngole, akiwaeleza viongozi hao kujiamini na kutembea kifua mbele wanapotekeleza majukumu ikiwa ni pamoja na kuwa karibu na wananchi kwa kusikiliza kero na kuzitatua.
 Katibu Mwenezi wa Kata ya Kidegembye, Fidelis Lyapanga akiuliza swali pamoja na kutoa maoni yake jinsi ya kuimarisha uhai wa chama wakati wa kikao hicho.
 Katibu wa Wazazi wa CCM Mkoa wa Njombe, Hussein Mwaikambo akisisitiza suala la kujenga umoja na ushirikiano miongoni mwa Jumuiya za chama ili kuimarisha uhai wa chama.
 Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi Kata ya Njombe Mjini, Solanus Mhagama akiuliza swali wakati wa mkutano huo.

 Katibu Mwenezi wa Kata ya Mfriga, Anangie akiuluza swali pamoja na kutoa shukrani kwa Katibu Mwenezi wa Mkoa, Ngole kwa mafunzo na maelekezo aliyowapatia wakati wa kikao hicho.
 Katibu Mwenezi wa Kata ya Mji Mwema Njombe, John Mtitu, akielezea mikakati mbalimbali wanayoifanya kuimarisha huai wa chama katika kata hiyo.
Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Njombe akiwa na maseneta viongozi wa CCM wa  Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Njombe baada ya kikao kumalizika. Viongozi hao walitambulishwa katika kikao hicho.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages