LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 20, 2020

KANISA HALISI LA MUNGU BABA LINAWAKARIBISHA WATU WOTE KWENYE HIJA YA CHANZO HALISI CHA MUNGU BABA, MJINI KIGOMA 26 THEBETI,1(26 APRILI,2020)

KWA NINI  HIJA MOJA HALISI IKO KIGOMA?
Sauti Mpya(2019) ambayo imetangaza kuwa Tanzania ni Taifa Baba ilisikika Kigoma–Tanzania; Sauti Mpya ambayo imetangaza kuwa Afrika ni Bara la Nuru ilisikika Kigoma–Tanzania; Sauti Mpya ambayo ni zaidi ya zile Sauti Saba ilisikika Kigoma-Tanzania; Sauti Mpya ambayo ni zaidi ya ishara tatu mbinguni (Ufunuo 12:1-9) ilisikika Kigoma–Tanzania; Sauti Mpya ambayo ni zaidi ya Nafsi ya Moyo (Miungu tisa mitakatifu iliyofafanuliwa ndani ya Kitabu) ilisikika Kigoma–Tanzania).

Sasa Kigoma, Tanzania na Afrika tujitambue kuwa tuna Sauti Mpya ambayo inabadilisha maisha mabaya kuwa mazuri. Sauti Mpya imebeba kila kitu kizuri. Hija hii ya Chanzo Halisi cha MUNGU BABA, mjini Kigoma, siyo maigizo wala usanii, ni halisi.

Sauti Mpya sasa imepokelewa katika mabara yote kwa utukufu wa MUNGU BABA. WATU WA DINI ZOTE; MADHEHEBU YOTE; MAKABILA YOTE; LUGHA ZOTE; NGAZI ZOTE; SEKTA ZOTE NA MATAIFA YOTE MNAKARIBISHWA BILA KUKOSA- LANGO LA 26 THEBETI,1 (26 APRILI,2020).

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages