LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 13, 2020

JUHUDI ZA KONGRESI ZA KUPUNGUZA UCHUMI WA VITA WA TRUMP

Baada ya bunge la Kongresi kupitisha mwasada wa kupanguza madaraka ya rais huyo kuhusiana na suala la kuanzisha vita na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sasa umefika wakati wa Seneti ya nchi hiyo kuchukua uamuzi katika uwanja huo. Katika hali ambayo Seneti ina wakati hadi kufikia mwisho wa leo Alkhamisi tarehe 13 Februari, kuchukua uamuzi kuhusiana na suala hilo, Trump kwa mara nyingine ameitaka itupilie mbali mswada huo, kwa hoja kuwa kupitishwa kwake kutadhoofisha madaraka ya rais wa Marekani na kutuma ujumbe dhaifu kwa Iran.
Kwa mara nyingine Trump amekariri madai yake yasiyo na msingi kuhusiana na mauaji ya kigaidi ya Soleimani na kudai kuwa Wamarekani wameridhishwa na hatua hiyo ya kigaidi. Amesema: Kama mikono yangu ungekuwa imefungwa Iran bila shaka ingekuwa na hali nzuri zaidi. Mswada huo unatoa ujumbe mbaya sana. Wademokrat wanachukua hatua hiyo kwa ajili tu ya kutoa pigo dhidi ya chama cha Republican. Msiruhusu jambo hilo litokee.'
Kwa mujibu wa mswada na azimio hilo linalotazamiwa kupigiwa kura leo usiku kwa majira ya Marekani, kibali cha vita dhidi ya Iraq ambacho kilitumiwa vibaya na Trump katika kumuua kigaidi Luteni Soleimani, kitafutiliwa mbali na kushuriutisha vita dhidi ya Iran kutekelezwa kwa ruhusa ya Kongresi. Kwa mujibu wa mswada huo uliowasilishwa na mbunge wa chama cha Demokrat, Tim Kaine, Trump atatakiwa kupunguza uhasama wote alionao na Iran katika kipindi cha siku 30, isipokuwa upitishwe na Seneti. Maneno yaliyotumika katika azimio hilo yamepangwa kwa njia maalum ambayo imekusudiwa kuvutia uungaji mkono wa maseneta wa Republican.

Tim Kaine, mbunge wa chama cha Democrat

Wakati wa kupasishwa azimio hilo katika bunge la Kongresi mnamo tarehe 9 Januari mwaka huu, ambapo wabunge 3 wa chama cha Republican pia waliuunga mkono, Trump alidai kuwa hatua hiyo itazidisha uwezekano wa kufichuliwa siri za shambulio la kijeshi dhidi ya Iran. Kwa msingi huo White Haouse inasisitiza kuwa iwapo azimio hilo litapitishwa katika Seneti, Rais Trump hatakuwa na budi ila kulipinga kwa veto. Nukta ya kuzingatia hapa ni kwamba maseneta wanane wa chama cha Republican wametaka kujadiliwa kwa kina mswada huo katika bunge hilo na kwa msingi huo iwapo utapigiwa kura kuna uwezekano mkubwa wa kupitishwa na bunge hilo la juu. Hata kama Waripublican wanakiri kwamba kuna tofauti za mitazamo katika chama hicho lakini wanajaribu kuonyesha kwamba uungaji mkono wa baadhi ya maseneta wa chama hicho kwa azimio hilo la Kaine si jambo kubwa.
Tim Kaine na wenzao ambao wamewasilisha azimio hilo wanasema kwamba, azimio hilo halimlengi Trump wala ofisi ya rais wa Marekani bali linasisitiza juu ya mamlaka ya Kongresi ya kutangazwa vita dhidi ya nchi nyingine. Huku akipinga madai ambayo yametolewa na Trump na wale wanaomuunga mkono, Kaine amesema kuwa ukweli wa mambo ni kinyume kabisa na inavyodaiwa. Wakati sote tutakaposisitiza juu ya kuzingatiwa sheria, na hasa katika ulimwengu wa leo ambao unahitaji kuwepo sheria zaidi, tukasema kuwa suala hili ni la kimuundo na kimsingi na kwamba kuna sheria ambazo tunapasa kuzichunga na kuzitii na wakati huo huo tukalazimika kuzifuata, hapo ndipo tutakuwa na haki ya kusema, hakika huo ndio uamuzi wa sawa.

Seneti ya Marekani

Wademokrat wanaamini kwamba hata kama Trump na marais wengine wa Marekani wanahitaji kuwa na uwezo wa kuilinda nchi dhidi ya mashambulio au uvamizi wa adui, uwezo huo unamalizikia hapo kwenye hujuma hiyo na kwamba uamuzi wa mwisho wa kuishambulia kijeshi nchi nyingine unapaswa kutolewa na Kongresi ya nchi hiyo na wala sio rais wa nchi. Kwa kutilia maanani mvutano mkubwa uliopo kati ya Wademokrat na Trump kuhusu masuala mengi ya Marekani, ni wazi kuwa kupitishwa azimio hilo katika Seneti ya Marekani itakuwa ni juhudi nyingine kati ya juhudi zinazofanywa na Kongresi ya Marekani kwa ajili ya kupunguza makali ya mashine ya vita ya Trump na timu yake ya uchokozi dhidi ya nchi nyingine.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages