LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 1, 2020

IRGC: MAJERUHI YA UBONGO' NI NJIA YA KUFICHA IDADI YA ASKARI WA MAREKANI

Katika makala aliyoandika katika gazeti la Vatan-e-Emrooz la Iran toleo la Jumamosi, Msemaji wa IRGC Brigedia Ramezan Shariff amesema: "Tumefikia natija kuwa wakati Marekani inaposema wanajeshi wake wamepata 'majeraha ya ubongo' kufuatia hujuma dhidi ya kituo cha Ain al Assad, kauli hiyo inamaanisha wanajeshi wa Marekani waliouawa."
Ameongeza kuwa, "naamini kuwa wanaposema 'majeraha ya ubongo' ni nukta inayoashiria idadi ya wanajeshi waliouawa lakini hawataki kutangaza rasmi idadi hiyo."
Brigedia Shariff amesema kwa mujibu wa taarifa, makombora 13 ya Iran yaliyolenga kituo hicho yalisababisha hasara kubwa na kupelekea idadi kubwa ya wanajeshi wa Marekani kuangamizwa katika oparesheni hiyo.

Makombora ya IRGC yakivurumishwa kuelekea katika kambi ya Ain al Assad ya Marekani nchini Iraq

Itakumbukwa kwamba tarehe 8 ya mwezi huu Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC lilitoa jibu kali ikiwa ni katika kujibu jinai za jeshi la Marekani baada ya kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha jeshi hilo la Iran. Katika jibu hilo IRGC ilishambulia kwa makombora kambi ya kijeshi ya Ain Assad ya Marekani nchini Iraq katika mkoa wa Al-Anbar.
Televisheni ya CNN juzi usiku ilitangaza habari kuhusu kuongezeka idadi ya wanajeshi wa Marekani waliojeruhiwa katika shambulio la Iran dhidi ya kambi ya kijeshi ya nchi hiyo ya Ain al Assad huko Iraq. CNN imewanukuu maafisa wawili wa Marekani na kutangaza kuwa hadi kufikia sasa wanajeshi wa Marekani wasiopungua 64 wamepata majeraha ya ubongo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages