LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 14, 2020

IDDI SIMBA AZIKWA LEO

  Msemaji wa Familia ya Marehemu Idd Simba, Ahmed Simba, amesema kuwa mwili wa Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara, utapumzishwa katika makaburi ya Mwinyi Mkuu Magomeni, lengo likiwa ni kumpumzisha mahali ambapo Baba zake wote walizikwa.


"Safari ilianzia Msasani nyumbani kwake, nakuondoka na mwili mpaka Msikiti wa Manyema uliposwaliwa kisha kuelekea Magomeni na kuzikwa katika makaburi ya Mwinyi Mkuu, amezikwa kule kwa sababu Baba zake wote wamezikwa hapo" amesema Ahmad.

Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara Iddi Simba, alifariki Dunia siku ya jana Februari 13, 2020, katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete alikokuwa akipatiwa matibabu, ambapo alihudumu nafasi yake kati ya mwaka 2001 na 2002.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages