LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 15, 2020

DK. BASHIRU AKERWA NA UBADHIRIFU WA FEDHA MOROGORO VIJIJINI

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dk. Bashiru Ally akimpokea aliyekuwa mwanachama na Diwani wa ACT- Wazalendo Kata ya Tomondo Khamis Msangule baada ya yeye na Diwani mwenzake kwa tiketi ya chama hicho Juma Manyile wa kata ya Selembala pamoja na viongozi mbalimbali wa chama hicho na Chadema, kutangaza kujivua uanachama wa vyama hivyo na kujiunga na CCM katika mkutano wa ndani wa viongozi wa mashina, Kata, wilaya na mkoa, uliofanyika  baada ya kutembelea Kituo cha Afya cha Mikese, Morogoro Vijijini akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Morogoro. KWA PICHA ZAIDI ZA ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM DK. BASHIRU MKOANI MOROGORO, TAFADHALI>>>  BOFYA HAPA

Na Said Said Nguya, Afisa Habari, Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ally ameonyesha kukerwa na ubadhirifu wa matumizi mabaya ya fedha Mikese, Morogoro Vijijini kwa fidia ya sh.milioni 300 ya majengo ya zahanati zilizotolewa na Kampuni ya ujenzi wa reli ya kisasa kutumika kujenga jengo moja tu wakati sh. milioni 300 zimetumika kujenga jengo moja, wakati sh. milioni 380 zilizokuwa zikisimamiwa na Halmashauri zimejenga majengo saba ya kituo hicho cha afya.

 Kufuatia kadhia hiyo, Dk. Bashiru amemwagiza Mkuu wa mkoa wa Morogoro Loatha Sanare kufuatilia ili kupata undani waliohusika wachukulie hatua kali ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Dk. Bashiru ametoa alitoa maagizo hayo jana, Februari 14, 2020, katika mkutano wa ndani wa viongozi wa mashina, Kata, wilaya na mkoa,  baada ya kutembelea Kituo hicho cha Afya cha Mikese, Morogoro Vijijini akiwa katika ziara ya kikazo mkoani Morogoro.

"Leo nimeenda Mikese nikaambiwa kuna kituo kimejengwa kama fidia ya Zahanati ambayo imepitiwa na mradi wa treni ya mwendo kasi eti thamani yake milioni 300, lakini majengo karibu saba yaliyoko pale yaliyojengwa na serikali kwa usimamizi wa Halmashauri ni sh. milioni 380, majengo saba, alafu wao chumba kimoja nilichokiona ni milioni 300."

Katibu Mkuu ametoa maelekezo kuwa, "Nimeona pale kuna shida, Mkuu wa Mkoa nakuelekeza, uchunguzi ufanyike pale, na waliofanya ubadhirifu huo washughulikiwe kwa mujibu wa sheria."

Wakati huo huo Dk. Bashiru amesisitiza suala la haki kwa wanachi ikiwa ni pamoja na haki ya watoto kupata elimu, malezi na mambo yote yanayohusu maisha ya watu, hivyo amewataka Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Ofisi zote za Umma kutenda haki kwa wananchi wote.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu amegusia kwa kuonya suala la baadhi ya wanachama kuanza kujipitisha katika majimbo na kata kabla ya wakati kwa kufanya vikao vya fitina na kuchafuana, hasa kwenye majimbo na kata za CCM. Amesisitza kuwa, kufanya hivyo ni kukiuka misingi ya haki, Chama hakitawavumilia wanachama hao.

Katika hatua nyingine, madiwani wawili wa ACT na Chadema Ndg. Khamis Msangule kata ya Tomondo na Juma Manyile kata ya Selembala pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama hivo, wamejivua uanachama wa vyama hivyo na kujiunga na CCM katika mkutano huo.

Katika ziara hiyo, Viongozi mbalimbali wameambatana na Katibu Mkuu wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Innocent Kalogeris pamoja na Mkuu wa Mkoa huoLoatha Sanare.

Katibu Mkuu yupo Mkoani Morogoro katika ziara ya siku tatu ambapo ametembelea wilaya za Kilombero na Morogoro Vijini, ambapo ziara hiyo imelenga katika kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kuimarisha Chama ngazi za msingi, pamoja na kujenga mahusiano baina ya viongozi wa Chama na serikali.


Imetolewa na;

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages