LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 12, 2020

DANIEL ARAP MOI AZIKWA LEO KABARAK

  Rais wa zamani wa Kenya, Daniel arap Moi, anazikwa leo kwenye mji wa nyumbani kwake wa Kabarak baada ya maelfu ya watu kushiriki jana ibada ya kutoa salamu za mwisho mjini Nairobi.


Mwili wa Moi uliwasili Kabarak mapema leo asubuhi na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya aongoza mamia ya watu kushiriki mazishi yake yoliyonyika mchana wa leo.

Wakati wa ibada ya taifa hapo jana Rais Kenyatta alimwelezea Moi kuwa kiongozi mpenda amani, baba wa taifa na kinara wa kupigania bara la Afrika pamoja na haki ulimwenguni.

 Moi aliyeiongoza Kenya tangu mwaka 1978 hadi 2002 alifariki wiki iliyopita akiwa na umri wa mika 95.

Hata hivyo utawala wa Moi aliyefahamika kwa jina la "Profesa wa Siasa" uliandamwa na visa vya rushwa na tuhuma za ukiukwaji mkubwa wa haki wa za binaadamu.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages