Na Yassir Simb,Michuzi Globu.
Uongozi wa Klabu ya Yanga imeitupia lawama bodi ya ligi (TPLB) kwa kubadilisha tena sehemu ya mchezo wao dhidi ya Wakulima wa Alizeti Singida United kutoka dimba la Sheikh Amri Abeid jijini Arusha na kuurejesha mpambano huo katika dimba la Namfua mkoani Singida, ikiwa ni muda mfupi tu baada ya wao wakiwa tayari wamefanya maandalizi ya awali.
Katibu Mkuu wa Yanga, Dk. David Luhago amesema tayari wamefanya maandalizi ya 'booking' ya usafiri wa ndege na kulipa sehemu ya pesa (advance) katika hoteli watakayo fikia, hivyo hawaelewi ni namna gani watarudisha gharama zao kufuatia mabadiliko hayo.
Dk. Luhago amesema kwa kawaida ikiwa kuna mabadiliko ya ratiba ya mchezo, taarifa inapaswa kutolewa saa 48 kabla lakin bodi ya Ligi haikufanya hivyo na kuwashtukiza kuwaambia mchezo huo utapigwa mkoani Singida nasi jijini Arusha tena.

"Bodi
ya ligi ilituandikia barua kuwa mchezo wetu dhidi dhidi ya Singida
United utapigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha lakini wamebadili
tena, kuwa tutaenda Singida katika uwanja wa Namfua wakati sisi
tushalipa gharama za awali,taarifa ilipaswa kutolewa mapema , sisi
tumejiandaa kuwa tunasafiri kwenda Arusha." alisema Dk Luhago.
No comments:
Post a Comment
ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇