LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 1, 2020

WAZEE WA MULEBA WAIPONGEZA CCM

Muleba, Tanzania
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amekutana na kufanya mazungumzo na taasisi ya KWA WAZEE iliyopo Muleba Mkoani Kagera.

Katika mazungumzo hayo, pamoja na mambo mengine, taasisi hiyo inayojumuisha wazee 29, 945 kutoka kila kata,  wameipongeza CCM kwa kuanzisha utaratibu wa Mabaraza ya Wazee katika kila ngazi na wao wameahidi kuwa mstari wa mbele kuhamasisha wazee wote wajiunge kwenye Mabaraza hayo ili changamoto zao zipate urahisi wa kusikilizwa na kutatuliwa kwa pamoja.

Mazungumzo hayo yamefanyika Leo tarehe 01 Januari, 2020 nyumbani kwa Katibu Mkuu Kemondo, Bukoba   vijijini.

Akizungumza, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bibi. Lydia Lugazia kwa niaba ya wazee wa taasisi hiyo amesema, 

"Sisi wazee tuliposikia CCM imeanzisha utaratibu huu wa Mabaraza ya Wazee kwenye kila ngazi, tulifarijika sana kwa kuwa sasa tutapata mahala sahihi zaidi pa kupeleka changamoto zetu kwa pamoja, na kwa kuwa sisi wa Muleba tulisha anza kukaa pamoja chini ya taaisis ya KWA WAZEE, tunaahidi kutoa ushirikiano na kuhamasisha wazee wote tuwe kwenye Mabaraza haya, Ili changamoto zetu zitatuliwe kwa pamoja."

Katika mazungumzo hayo, Dkt. Bashiru amewahakikishia nia ya dhati ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. John Pombe Magufuli kuunda mabaraza hayo ni kuwa karibu zaidi na wazee na siku zote amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha changomoto zenu mbalimbali zikiwemo za Afya zinatatuliwa.

Katibu Mkuu Mkuu yupo Nyumbani kwake Bukoba kwa mapumziko, ambapo anatarajiwa kumaliza mapumziko hayo mapema mwezi Januari, 2, 2020

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages