Wakati huohuo nchi hiyo imeweka katazo kali la kusafiri ili kuzuia maambukizi zaidi.
Mji wa Wuhan, ambao unaelezwa kuwa chanzo cha maambukizi ya virusi.
Idadi ya walioambukizwa kimataifa imeongezeka kukiwa na taarifa za maambukizi mapya huko Singapore na Ujerumani.
Nchini China, miji mikubwa kadhaa imesitisha huduma ya usafirishaji wa Umma.
Mlipuko wa ugonjwa huu umekuja wakati wa sherehe za mwaka mpya ambazo huwakutanisha mamilioni ya watu nchini humo wakisafiri kuwatembelea ndugu na marafiki.
Sherehe za mwaka mpya zilisogezwa mbele kwa siku tatu mpaka siku ya Jumapili, ili kudhibiti kuenea kwa maambukizi.
Marekani, ambayo ina maambukizi ya watu kadhaa, imewataka raia wake ''kufikiria upya suala la kusafiri'' kwenda China na imeshauri kutosafiri kwenda Hubei.
Nchi nyingine nyingi zimetahadharisha safiri za kwenda China huku wengine wakipanga kuwasafirisha raia wao waliokwama mjini Wuhan.
Mpaka sasa hakuna vifo vilivyoripotiwa nje ya China.
Virusi vya corona vilianza lini?
Virusi hivi havijawahi kutokea kabla ya mwezi disemba mwaka 2019 na vikapewa jina la "novel coronavirus".
Virusi vya aina hii huwa kwa kawaida vinawaathiri wanyama lakini mara nyingine, vinaweza kuwapata binadamu, kwa mfano mlipuko wa ugonjwa wa 'Sars' ambao uliuwa watu wengi China.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇