LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 18, 2020

UNICEF YATAHADHARISHA KUHUSU HALI MBAYA WANAYOKABILIWA WATOTO LIBYA

Henrietta H. Fore, Mkuu wa Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa ametangaza katika taarifa yake aliyoitoa hapo jana kwamba, watoto wa Libya wangali wanataabika sana kwa vitendo vya utumiaji mabavu na vita vya ndani vinavyoendelea kushuhudiwa katika nchi hiyo.
Mkuu huyo wa Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, kuanzia Aprili mwaka jana hali ya maelfu ya watoto nchini Libya imekuwa mbaya sana baada yay kuanza mashambulio ya vikosi vitiifu kwa Jenerali Khalifa Haftar. Aidha amesema kuuwa, roho za mamia ya watoto wa Libya zimepotea kufuatia kushadidi hali ya ukosefu wa usalama katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Ripoti zaidi zinasema kuwa, watoto wa Libya wamekuwa wakiuawa na wengine kutumiwa vibaya katika medani ya vita.
Baada ya kupinduliwa utawala wa Kanali Muammar Gaddafi huko Libya mwaka 2011, nchi hiyo ilitumbukia katika vita vya ndani na hivi sasa kuna serikali mbili hasimu, moja ya mashariki na nyingine ya magharibi mwa nchi hiyo ambapo vikosi vya pande hizo mbili vinaendelea kupigana,
Tokea Aprili mwaka jana wakati Haftar alipoanzisha vita dhidi ya mji mkuu Tripoli, watu wasiopungua 1,100 wameuawa, zaidi ya 5700 wamejeruhiwa na zaidi ya 146,000 kuachwa bila makao.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages