LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 5, 2020

MWILI MTOHARIFU WA SHAHIDI LUTENI JENERALI QASSM SOLEIMANI WAWASILI IRANI YA KIISLAMU

Mamia ya watu wamefika katika uwanja huo wa ndege kuupokea mwili wa Shahidi Qassem Suleimani na ule wa Abu Mahdi la Muhandis, Kamanda wa Kikosi cha Hashd al Shaabi cha Iraq pamoja na wanajihadi wenzao waliouawa Ijumaa katika hujuma ya kigaidi ya Marekani mjini Baghdad.
Siku ya Jumamosi kulifanyika maandamano ya mazishi ya mashahidi hao katika miji ya Kadhimein, Baghdad, Karabala na Najaf nchini Iraq.
Miili ya mashahidi ikiwasili Iran
Kwa mujibu wa ratiba, leo mjini Ahavaz, mkoani Khuzestan, kutafanyika shughuli ya mazishi na kuwaaga mashahidi hao wa muqawama.
Baadaye leo adhuhuri shughuli ya mazishi itaendelea katika Haram Takatifu ya Imam Ridha AS, Imam wa nane wa Mashia katika mji wa Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran. Miji mingine ambayo kutafanyika shughuli ya mazishi na kuwaaga mashahidi hao ni Tehran, Qum na hatimaye maziko yamepengwa kufanyika Kerman alikozaliwa Shahidi Luteni Jenerali Soleimani.
Luteni Jenerali Qassem Solaimani na naibu mkuu wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al Hashdul Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes waliuawa shahidi mapema Ijumaa katika shambulizi la Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq.
Wizara ya Ulinzi ya Marekani imetangaza kuwa, Rais Donald Trump wa nchi hiyo ndiye aliyetoa amri ya kuuliwa shahidi Jenerali Qassem Soleimani.  

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages