Dar es Salaam.
Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), limetangaza matokeo ya upimaji kitaifa darasa la nne, kidato cha pili na nne ya mitihani iliyofanyika Novemba 2019.
Matokeo ya kidato cha nne mwaka 2019 yanaonyesha kuwa ufaulu umeongezeka kidogo kwa asilimia 1.4 kutoka ule wa mwaka 2018. Licha ya ufaulu huo kuongezeka, bado takriban nusu ama asilimia 48.6 ya watahiniwa wote wa mwaka 2019 wamepata daraja la nne.
Necta imeeleza leo kuwa katika mtihani huo wanafunzi 340,914 wamefaulu mtihani kati ya wanafunzi 422,722 waliofanya mtihani huo Oktoba mwaka jana ikiwa ni sawa na asilimia 80.65 ya watahiniwa wote.
Hii ni sawa na kusema kuwa wanafunzi 81 kati ya 100 waliofanya mtihani huo wamefaulu.
Ufaulu huo, kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde, ni sawa ongezeko la asilimia 1.38 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2018. Mwaka juzi asilimia 79.27 ya watahiniwa wa shule walifaulu mtihani huo. Kuona matokeo Kidato cha Nne,BOFYA HAPA
🤔
ReplyDelete