<Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, Benjamini Sitta na Luteni Kanali wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) David Luoga (kushoto), walipokuwa wakitia saini Mkataba wa JWTZ kujenga Jengo la Utawala na Uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu, jana.
KINONDONI, Dar es Salaam
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imesaini mkataba na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya JWTZ kujenga Uwanja wa wa kisasa wa mpira wa miguu na Jengo la kisasa la Utawala la Halmashauri hiyo.
Mkataba huo umesainiwa jana na Mstahiki Meya wa Halmashauri hiyo Benjamini Sitta na Luteni Kanali David Michael Luoga na kushuhudiwa na watendaji wa Halmashauri hiyo pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kinondoni Harlod Maruma.
Akizungumza na wandishi wa habari wakati wa utiaji saini wa mkataba huo, Meya Sitta amesema kuwa mradi wa ujenzi wa jengo la utawala utagarimu kiasi cha sh. Bilioni 1.6 huku ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu ukigarimu kiasi cha sh. Bilioni 2.7.
Amefafanua kuwa uamuzi wa kutumia JWTZ umetokana na kufuata ushauri uliokuwa unatolewa na Rais Dk. John Magufuli wakutumia Locol Fundi (Foce Account).
Meya amesema kuwa miradi hiyo mikubwa miwili iliyosainiwa jana itajengwa na Jeshi la Wananchi kwakuwa wana amini watafanya kazi hoyo kwa umakini mkubwa na wa haraka kulingana na mkataba huo ulivyoeleza.
“ Tunamshukuru Rais wetu mpendwa, Dk. Magufuli kwa kutuonyesha njia ya kufanya kazi kwa kutumia wanajeshi kwa kuwa itakamilika kwa wakati, hapa hakuna michakato, miradi hii mikubwa itafanywa na jeshi la JWTZ” amesema Meya Sitta.
Aidha Meya Sitta amesema “ tunampongeza Mkurugenzi wetu Aron Kagurumjuli, kwakweli tuna mkurugenzi makini, msikivu ,ambaye anafuata maelekezo na ni mchapakazi ndio mana leo Kinondoni yetu ipo hapa” ameongeza.
Kwa upande wake Luteni Kanali Luoga ameipongeza Manispaa ya Kinondoni kwa kuwaamini kufanya kazi hiyo na kuahidi kukalimisha ujenzi huo kwa muda wa miezi sita.
Luteni Luoga amesema katika ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu, awamu ya kwanza itakamilika kwa kipindi cha miezi mitatu na nusu na awamu ya pili itatumia miezi miwili na nusu.
Ameongeza kuwa katika ujenzi huo ,licha ya kwamba Jeshi la Wananchi litafanyakazi hiyo,lakini pia litatoa nafasi kwa watu wengine ikiwemo Mama ntilie pamoja na vijana wengine lengo likiwa ni kila mwananchi apate kipato.
“ Tunampongeza Mhe. Meya Sitta, Mkurugenzi Kagurumjuli kwa kutuamini, nasisi tunawahakikishia kuwa Jengo la utawala pamoja na uwanja tutakamilisha kwa kipindi cha miezi sita kama ilivyo kwenye mkataba wetu”amesema Luteni Kanali Luoga.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Mhe. Harlod Muruma amefafanua kuwa ujenzi huo wa miradi mikubwa miwili iliyotiwa saini leo ni utekelezaji wa ilani CCM.
Your Ad Spot
Jan 28, 2020
Home
featured
Uchumi
MANISPAA YA KINONDONI YASAINI MKATABA WA ZAIDI YA SH. BILIONI 3 UJENZI WA UWANJA W A KISASA NA JENGO LA UTAWALA
MANISPAA YA KINONDONI YASAINI MKATABA WA ZAIDI YA SH. BILIONI 3 UJENZI WA UWANJA W A KISASA NA JENGO LA UTAWALA
Tags
featured#
Uchumi#
Share This
About Bashir Nkoromo
Uchumi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇