Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara), Philip Mangula akihutubia katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM
Wilaya ya Wanging’ombe, mkoani Njombe uliofanyika Januari 03/2020 kwa lengo la kutoa na
kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Mangula akikabidhiwa zawadi ya mbuzi
Mangula (katikati), akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi wa CCM alipokwenda kufungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM
Wilaya ya Wanging’ombe uliofanyika Januari 03/2020 kwa lengo la kutoa na
kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Na Maiko Luoga Njombe,
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Tanzania bara Ndg, Philip Mangula amewataka wanachama na Viongozi wa CCM Nchini kuzingatia Kanuni na taratibu za chama hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais.
Mangula ametoa agizo hilo katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Wanging’ombe uliofanyika Januari 03/2020 kwa lengo la kutoa na kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Akihutubia Wanachama walioshiriki Mkutano huo wa kupokea Taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani Wanging’ombe kwa mwaka 2019 amesema, Kamati za siasa zitawajibika endapo ukiukwaji wa kanuni utajitokeza na kuongeza kuwa endapo wataachwa Viongozi hao watahatarisha hali ya Amani na utulivu ndani ya Chama.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Wanging’ombe wamekutana katika Kikao cha kutathmini na kupokea Taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama ambayo imewasilishwa kwao na Mkuu wa Wilaya hiyo Comrade Ally Kasinge na Mbunge wa Jimbo Mhe, Gerson Lwenge.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Philip Mangula alikuwa Mgeni rasmi katika Mkutano huo, pia ametoa angalizo kwa Wanachama wa CCM nchini kujiepusha na uvunjwaji wa kanuni na Taratibu za chama kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Nchini mwaka huu 2020.
Awali wakisoma Taarifa ya utekelezaji wa Ilani, Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe Ally Kasinge na Mbunge wa jimbo hilo Muhandisi Gerson Lwenge wamekili kupokea fedha za miradi ya maendeleo ya Maji na Elimu kutoka Serikali kuu huduma ambazo awali zilikuwa kero kwa wakazi wa Wilaya hiyo.
Pamoja na kuridhishwa na utatuzi wa kero za Wananchi, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe kupitia Mwenyekiti wake Mzee Jassel Mwamwala, wametumia fursa hiyo kuwahimiza Wananchi kujitokeza kujiandikisha na kuboresha Taarifa zao katika Daftari la kudumu la Mpiga kura lililoanza Mkoani hapa Januari mosi na kutarajiwa kuhitimishwa Januari 07/2020.
Akizungumza kwa Niaba ya Wananchi na Wanachama wa Wilaya ya Wanging’ombe Katibu wa CCM Wilayani humo Ndg, Juma Nambaila amemshukuru Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara kwakuhudhuria Mkutano huo na kuridhishwa na Utekelezaji wa Ilani katika Wilaya hiyo.
Viongozi wengine wa CCM Mkoa wa Njombe walioshiriki Mkutano huo ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kutoka Mkoa wa Njombe Ndg, Fidelis Lumato, na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa Ndg, Erasto Ngole.
Wengine ni Mwenyekiti wa UVCCM Ndg, Nehemia Tweve na Katibu wake Ndg, Amosi Kusakula, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Mkoa Ndg, Seneta Mwaikambo na Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Njombe.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇