Waziri Ummy Mwalimu akiangalia kipimo cha uchunguzi wa saratani ya
matiti'Mammography' kilichopo kwenye kwenye hospitali ya Benjamin Mkapa
Na. Catherine Sungura-Dodoma
Hospitali ya
Benjamin Mkapa imetakiwa kujiunga na tiba mtandao ili kuweza kutoa tiba
kwa wagonjwa kwa haraka na kwa ufanisi ili kuwapunguzia wagonjwa muda
wa kusubiri majibu hususani ya mionzi .
Rai
hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Ummy Mwalimu wakati alipoitembelea hospitali hiyo kujionea
hali ya utoaji huduma.
“Nawaelekeza ni vyema
mkajiunga na huduma ya tiba mtandao ili muweze kutoa huduma kwa haraka
na kwa ufanisi zaidi, mnatakiwa mkajifunze huduma hii kutoka hospitali
ya Muhimbili au MOI". Amesema waziri Ummy.
Aidha,
Waziri huyo amesema kuwa hivi sasa kwenye hospitali nyingi kuna
changamoto za wataalam wa kusoma picha kwani wataalam wengi waliopo ni
wale wa kupiga ”bahati nzuri sisi tunao wataalam wengi wa kupiga picha
mana kwenye mionzi kuna aina mbili za wataalam wapo wa kupiga picha
(radiographer) na wa kusoma picha, hivyo serikali itahakikisha inapata
wataalam wengi zaidi wa kusoma ili kukidhi mahitaji.
Waziri
Ummy amesema wizara ina lengo la kuziunganisha hospitali za wilaya
pamoja na vituo vya afya kwenye mfumo wa hospitali za rufaa za mikoa kwa
kufunga senta zitakazosaidia hospitali za wilaya na vituo vya afya
vinavyofanya vipimo vya ‘utra sound’ na ‘x-ray’ na majibu yakasomwa
haraka na wataalam wa Hospitali za rufaa na kutoa majibu haraka bila
kumsubirisha mgonjwa kwa muda mrefu.
Alitaja
hospitali zilizojiunga na tiba mtandao ni pamoja na hospitali za rufaa
za mikoa ya Lindi na Morogoro , pia hospitali teule za wilaya za
Nyangao,Turiani na hospitali za wilaya ya Nachingwea,kilosa na Mvomero.
Wakati
huo huo Waziri Ummy ameitaka hospitali hiyo kupunguza gharama za
kulipia uchunguzi wa saratani ya matiti kwa wanawake kutoka elfu sabini
hadi elfu thelathini kama hospitali zingine za taifa zinavyofanya.
Hata
hivyo waziri huyo ametoa wito kwa wananchi wa Dodoma na mikoa jirani
kutosafiri hadi dar es salaam kupata huduma za kibingwa kwani huduma
zote karibu zinapatikana hapo na hivyo ameahidi wizara wataleta
madaktari bingwa wa mishipa ya fahamu pamoja na mifupa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇