MKUU wa Wilaya ya Busega,Tano Mwera ametoa wito kwa Wananchi wote wa Mji wa Lamadi na maeneo ya jirani kujitokeza kupata namba ya utambulisho wa Uraia (NIDA).
Zoezi hilo litaendeshwa kwa siku tatu na maafisa wa NIDA ambao wamepga kambi mjini humo
"Nachukua nafasi hii kuwahamasisha wana Lamadi wote ambao wanataka namba ya utambulisho wa Uraia (NIDA), Wafike katika ofisi ya Mtendaji wa Kata kwa wingi na watapata huduma hiyo kwa siku tatu" alisema DC Tano Mwera.
Aidha, Mkuu wa Wilaya huyo amesema kuwa baada ya zoezi hilo la muda wa siku tatu kumalizika katika mji huo wa Lamadi na maeneo jirani ikiwemo Mkula, Wananchi wataifuata huduma hiyo Nyashimo, Wilayani.
"Tunamshukuru Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa kuongeza muda wa zoezi la Usajili wa namba kwa alama za vidole.
Wafanyakazi wa NIDA hapa Busega wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kila mtu anapata namba yake. Tujitokeze kwa wingi kupata namba hizo" alisema DC Tano Mwera.
Zoezi hilo la NIDA linaendeshwa Nchi nzima ambapo kwa Wilaya ya Busega linaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇