LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 12, 2020

BALOZI WA UINGWREZA MJINI TEHRAN AWEKWA KIZIWIZINI

Balozi wa Uingereza mjini Tehran awekwa kizuizini
Balozi wa Uingereza mjini Tehran, Rob Macaire, atiwa nguvuni akishiriki shughuli iliyoandaliwa kuwakumbuka wahanga  wa ndege ya abiria ya Ukraine iliyoanguka mji mkuu wa Iran, Tehran.
Katika shughuli hiyo ambayo ilifanyika mbele ya chuo kikuu cha Emir kabir, kauli mbalimbali za kuipinga serikali zilikuwa zikatolewa na inasemekana kwamba Balozi Macaire alijaribu kuandaa vitendo vya uchochezi.
Pamoja na hayo balozi huyo aliachwa huru baada ya masaa kadhaa.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Dominic Raab alisema, “ Kuwekwa kizuizuni kwa balozi wetu mjini Tehran bila hatia wala maelezo ni uvunjifu wa sheria za kimataifa”.
Marekani nayo imeonyesha kupinga tukio hilo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani, Morgan Ortagus, alisema  " Tunatoa wito kwa Ä°ran, iombe radhi rasmi kwa Uingereza kutokana na uvunjifu wa haki na pia iheshimu haki za wanadiplomasia wote”

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages