Rais Donald Trump wa Marekani amekiri kuhusu hatua ya kijinai aliyochukua ya kuamuru kutekelezwa operesheni ya mauaji ya kigaidi dhidi ya kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC).
Katika kutetea na kuhalalisha amri aliyotoa ya kufanywa operesheni ya mauaji ya kigaidi dhidi ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani, kamanda wa kikosi cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Trump amedai kuwa, amechukua hatua hiyo kwa ajili ya kuzuia kutokea vita na akaongeza kwamba, Marekani imejiandaa kuchukua hatua nyingine yoyote dhidi ya Iran.
Rais wa Marekani vile vile amedai kuwa Marekani haitaki kubadilisha utawala nchini Iran na kwamba utumiaji vikosi vya niaba unaofanywa na Iran inapasa usitishwe mara moja.
Luteni Jenerali Qassem Soleimani, kamanda wa kikosi cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, aliuawa shahidi usiku wa kuamkia jana Ijumaa katika shambulio la kigaidi la anga lililofanywa na majeshi vamizi na ya kigaidi ya Marekani katika uwanja wa ndege wa Baghdad, ulioko kwenye mji mkuu huo wa Iraq.
Kufuatia jinai hiyo ya kinyama ya Marekani na ya ukiukaji sheria za kimataifa, Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran limetoa taarifa maalumu na kueleza kwamba, limeshapitisha maamuzi yanayostahiki kutekelezwa kujibu jinai ya mauaji ya kigaidi ya Luteni Jenerali Soleimani iliyofanywa na utawala wa Marekani na kusisitiza kuwa, jinai hiyo itakabiliwa na kisasi kikali katika wakati na mahala muafaka.../
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇