LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 10, 2019

YANGA SC KUFANYA ZIARA YA MECHI MBILI ZA KIRAFIKI KIGOMA WIKI IJAYO


Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KLABU ya Yanga SC inatarajiwa kufanya ziara ya mechi za kirafiki mkoani Kigoma wiki ijayo kipindi hiki Ligi Kuu ya Tanzania Bara ikiwa imesimama kupisha michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge iliyoanza jana nchini Uganda hadi Desemba 19.
Afisa Habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli amesema kwamba kikosi kitaondoka Alhamisi kwenda Kigoma na kitacheza mechi ya kwanza Ijumaa dhidi ya Mwamgongo FC na mwingine Jumapili dhidi ya Mbao FC Uwanja wa Lake Tanganyika.
Kocha wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa anataka kutumia mechi hizo kama sehemu ya maandalizi ya mechi ya hatua ya 32 Bora michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) dhidi ya Iringa United ya Daraja la Kwanza kati ya Desemba 20 na 22 Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.

Vigogo wa soka nchini, Azam FC na Simba nao wataanzia nyumbani pia hatua ya 32 Bora michuano hiyo maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
Mabingwa watetezi Azam FC, watakutana na African Lyon Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam na mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba SC watamenyana na AFC ya Arusha.
Hatua hii inashirikisha jumla ya timu 64, kati ya hizo 20 zinatoka Ligi Kuu ya Tanzania Bara, 24 kutoka Daraja la Kwanza na 20 nyingine ni madaraja ya chini zilizofuzu kutoka hatua za awali.
Mechi nyingine za michuano hiyo inayojulikana kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) ni kati ya Migombani dhidi ya Mbeya City, Polisi Tanzania na Top Boys, Mwadui FC na Mkamba Rangers, Tukuyu Stars na Singida United, Mbuni FC dhidi ya KMC, Alliance itamenyana na Transit Camp, Ndanda SC na Cosmo Politan na Milambo FC dhidi ya Ruvu Shooting.
Nayo Mbao FC itamenyana na Stand United, Nyamongo na Biashara United, Lipuli FC na Dar City, Kagera Sugar na Rufiji United, Tanzania Prisons na Mlale FC, Mtibwa Sugar na Rhino Rangers, Coastal Union na African Sports, Namungo FC na Green Warriors na JKT Tanzania dhidi ya Boma FC.
Mechi nyingine ni Migombani dhidi ya Mbeya City, Polisi Tanzania na Top Boys, Mwadui FC na Mkamba Rangers, Tukuyu Stars na Singida United, Mbuni FC na KMC, Alliance na Transit Camp, Ndanda SC na Cosmo Politan, Milambo FC na Ruvu Shooting, Mbao FC na Stand United na Nyamongo dhidi ya Biashara United.
Mawenzi Market itamenyana na Mtwivila, Mpwapwa United na Kitayosa, Talinega FC na Friends United, Ihefu na Kasulu Red Star, Toto Africans na Gipco, Mighty Elephant na Mashujaa FC, Jeshi Warriors na Dodoma FC, Majimaji FC na Pamba SC, Panama FC na Area C na  Gwambina FC dhidi ya Mbeya Kwanza.
Nayo Pan African itamenyana na Geita Gold, Njombe Mji na Sahare All Stars, Lipuli FC na Dar City, Kagera Sugar na Rufiji United, Tanzania Prisons na Mlale FC, Mtibwa Sugar na Rhino Rangers, Coastal Union na African Sports, Namungo FC na Green Warriors na  JKT Tanzania dhidi ya Boma FC.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages