Watu wasiopungua 11 wameuawa katika mapigano kati ya wanamgambo na wafanya biashara katika wilaya moja huko Bangui mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Duru za usalama na Imam wa msikiti kwa jina la Awad al Karim wameeleza kuwa miili 16 ya watu waliouliwa ilipelekwa katika msikiti wa Ali Babolo.
Mapigano hayo yalianza baada ya wafanya biashara kutoka katika wilaya ya PK5 yenye wakazi wengi wa Kiislamu kubeba silaha ili kupinga kodi zilizoainishwa na makundi ya wanamgambo. Bili Aminou Alao msemaji wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSCA amesema kuwa tayari wametuma kikosi chao cha radiamali ya haraka katika eneo palipojiri mapigano.
Mkuuu wa kikosi cha huduma za ulinzi kwa raia cha Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema kuwa sehemu ya soko na baadhi ya magari yamechomwa moto kwenye mapigano hayo. Kati ya maduka 40 hadi 50 yameungua pamoja na nyumba tano.
Jamhuri ya Afrika ya Kati imekuwa katika hali ya mchafukoge tangu mwaka 2014 baada ya Rais wa wakati huo wa nchi hiyo Francois Bozize kupinduliwa madarakani. Mgogoro wa muda wa nchi hiyo umesababisha karibu robo ya jamii ya watu nchi hiyo kuyahama makazi yao.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇