LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 23, 2019

UJENZI DARAJA LA DAR HADI ZANZIBAR


Mwenyekiti wa Baraza la Diaspora Duniani (TDC Global) Mhe Norman Jasson amesema kuwa Watanzania waishio nchi za nje (#Diaspora) wapo kwenye mkakati wa kujenga daraja lenye urefu wa takribani Kilomita 30.01 kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar na sasa wanasubiri baraka za serikali ili kuanza upembuzi yakinifu ili kujua gharama za ujenzi wa daraja hilo.

Daraja hilo litakuwa na njia tatu, moja ni kupitisha magari yanayotoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar na njia ya pili ni magari yanayotoka Zanzibar kuja Dar es Salaam na njia ya tatu ni kwa ajili ya watembea kwa miguu na waendesha baiskeli.

Mapendekezo matatu ya ujenzi wa daraja hilo yametolewa ambayo ni moja, kujenga daraja la kupita ndani ya bahari, pili daraja la kupita juu na tatu ni daraja linaloelea majini ambalo ndilo lililopendekezwa na ujenzi wake ni rahisi maana hutengenezwa nchi Kavu na kusafirishwa na meli na kisha kuunganishwa.

Daraja la ndani ya maji halikuchaguliwa kwasababu ndani ya maji Dar hadi Zanzibar kuna mkondo wa maji na maporomoko.

Daraja la juu halikuchaguliwa kwasababu bahari ya Hindi eneo hilo kuna kina kirefu.

Daraja la kuelea limechaguliwa kwasababu ujenzi wake ni rahisi na gharama zake ni nafuu na garantii yake ni miaka 100.

Diaspora wameamua kujenga daraja hilo kuunga mkono juhudi za Rais John Pombe Magufuli ili kurahisisha usafiri kati ya Dar es Salaam na Zanzibar na watalii waweze kusafiri hata kwa baiskeli.

Mwandishi toka Zanzibar
 
 
 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages