LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 20, 2019

TUGHE YAYOA TAMKO JUU YA ONGEZEKO LA ADA YA LESENI YA TAALUMA KWA MADAKTARI, WAUGUZI NA WAFAMASIA YAOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI





 Mwenyekiti TUGHE Taifa, Archie Mntambo akizungumza na Wajumbe wa Baraza Kuu TUGHE Taifa (hawapo pichani) Mkoani Morogoro uliofanyika katika Ukumbi wa EDEMA Desemba 20, 2019. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

NA KHAMISI MUSSA

CHAMA  cha wafanyakazi wa
Serikali na Afya  (TUGHE), kimepinga ongezeko ya ada ya kupata leseni ya taaluma ambayo inapandishwa  kwa wataalam ambao ni Madaktari, Wauguzi na Wafamasia.

Haya yalisema  na Mwenyekiti TUGHE Taifa, Archie Mntambo wakati alipokuwa  akizungumza na Wajumbe wa Baraza Kuu la wafanyakazi hao  lililofanyika kuanzia 19-20, Disemba 2019) Mkoani Morogoro.

Alisema wao pamoja na waauguzi, madaktari, wafamasia ambao ni wanachama   wa tughe hawapingi kulipia leseni bali ongezeko la ada ndio kikwazo kwao.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa wanapinga ada  inayoongeazwa na mabaraza ya kitaluma ili kupata Leseni za taaluma hizo. 

Mntambo aliongeza kuwa ada  ya leseni sasa imechukua nafasi zaidi kuliko taaluma yenyewe  na  kwamba kama  chama jukumu lake kubwa ni kutetea haki za wafanyakazi kwa mujibu wa sheria za nchi hivyo wanapinga jambo hilo.

"Leo hii hayo mabaraza yanaweka ada kubwa hali wakijua kwamba mfanyakazi huyu wa Tanzania mshahara haujapandishwa kwa kipindi kirefu hivyo ongezeko la ada hizo kunaongeza ugumu wa maisha kwa watumishi  na wanachama wetu," alisema Mwenyekiti huyo.

Alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Magufuli  amekuwa na msisitizo wa TUGHE kushirikishwa katika maeneo mengi,  na kwamba Rais amewashirikisha katika eneo la Kikokotoo na ametaka twende mbali zaidi tufike mahali tuone kama ni Kikokotoo gani cha jinsi gani ambacho kina maslahi na Mfanyakazi  Mtanzania mwenye maisha  ya chini.

Alisema Rais Magufuli  anafikiria mambo makubwa juu yao lakini kuna watu wachache wanatoa maamuzi yasiostahili ili tufike mahali tuanze kufikiria kitu kibaya juu ya Serikali yetu.

"Tunaimani na Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tunaimani na Waziri anaye simamia Sekta ya Afya na tunajuwa jabo hili hata linyamanzia kimya na sisi hatuta fikiria mabaya juu ya serikali yetu kwani tunaimani na Serikali.,"alisena

Alisema Mntambo kuwa ni matarajio yake  kuanzi leo zile sekta zote zinazohusiana na TUGHE kwenye maswala yote ambayo yana maslahi na watumishi watahusisha Chama cha Wafanyakazi.

Mwenyekiti huyo alitoa rai kwa wale wote waliopewa mamlaka, wanapoamua kufanya kitu chochote kinachohusiana na maslahi ya Mtumishi lazima watushirikishe TUGHE na vyama vingine kwa sekta husika.

Mungu Ibariki Tanzani Mungu tubariki Watanzania na asanteni kwa kunisikiliza.


   Mwakilishi wa Walemavu TUGHE Taifa, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Baraza Kuu (KUBK), Mjumbe wa Baraza Kuu na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TUGHE Taifa, Bi Honorina Banzi, alisema anafurahishwa na kasi ya Mh. Rais Magufuli ya kujenga uchumi, vilevile  "nimefurahishwa kuona Watu Wenye Ulemavu kupewa kipaumbele katika nafasi za juu hasa Naibu Waziri anayeshughulikia masuala ya Watu Wenye Ulemavu na viongozi wengine mbalimbali, hii ni hatua kubwa, ninafarijika sana sana na ninampongeza sana Mh. Rais"

















  Wajumbe wkiwa katika Ukumbi wa EDEMA uliopo Morogoro.
Mwenyekiti TUGHE Mkoa wa Pwani akizungumza katika Mkutano huo na akatumia nafasi ya kuishukuru Serikali ya Tanzania hasa kwa kipindi hiki cha awamu ya Tano ikiongozwa na Jemedari wa Mapambano anayepigania wanyonge ambaye ametusaidia sana vyama vya wafanyakazi, kwakuhimiza mabaraza ya wafanyakazi kuweza kufanyika sehem za kazi

Hii imetusaidia kwa wafanyakazi kujuwa umuhim wa vyama vya wafanyakazi, tumekuwa tukifanya mabaraza ya wafanyakazi huku tukiibua matatizo mengi ambayo wafanyakazi walikuwa wakiogopa kupoteza ajira zao lakini Rais wetu amekuwa muuungwana na amekuwa akipenda kituhiki kiwe wazi

Ofisi zote na wanachama wote wanaofanya kazi Tanzania wana Mabaraza na wanamabaraza mahala pa kazi japo yapo maeneo machache yanajitahiidi hili kwa pamoja, kwahiyo mimi ninapenda kumshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kuhimiza hili kwa wafanyakazi na Mungu ambariki na kuwabariki wasaidizi wake katika kutimiza majukum

Wanachama wakiimba wimbo wa Chama hicho






 Mwenyekiti TUGHE Taifa, Archie Mntambo (kushoto) akizumgumz jambo kabla ya kufunga Mkutano huo




Baadhi ya Wajumbe wakifurahia jambo huku wakiimba wimbo, Tunaimani na Rais Oyaoyaoya!, Rais kweli!  Kweli kwelikweli Rais, Rais kweli kweli huku wakipiga meza kwa furaha na nderemo  mara baada ya Mwenyekiti TUGHE Taifa, Archie Mntambo (hayupo pichani) kufunga Mkutano Kuu TUGHE Taifa na kutoa tamko rasmi Mkoani Morogoro leo Desemba 20, 2019
 Baadhi ya Wajumbe wakifurahia jambo huku wakiimba wimbo, Tunaimani na Rais Oyaoyaoya!, Rais kweli!  Kweli kwelikweli Rais, Rais kweli kweli huku wakipiga meza kwa furaha na nderemo  mara baada ya Mwenyekiti TUGHE Taifa, Archie Mntambo (hayupo pichani) kufunga Mkutano Kuu TUGHE Taifa na kutoa tamko rasmi Mkoani Morogoro leo Desemba 20, 2019


 Naibu katibu mkuu nd. Amani Msuya (kushoto) na Afisa Elimu wa Chama Nd. Nsubisi Mwasandende wakiwa katika Sala fupi ambayo iliongozwa na Mwenyekiti TUGHE Taifa, Archie Mntambo (hayupo pichani) kabla ya kuanza Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa EDEMA Mkoani Morogoro Desemba 20, 2019.
 Katibu wa Mkoa TUGHE Morogoro sara Rwezaula (kulia) akizungumza jambo na Katibu Mkuu TUGHE Hery Mkunda mara baada ya kufungwa rasmi Mkutano Mkuu Taifa leo Desemba 20, 2019
Mwenyekiti TUGHE Mkoa wa Morogoro Mohamed Simbeye (kushoto) akizungumza jambo na  Mwenyekiti TUGHE Taifa, Archie Mntambo mara baada ya kufunga Mkutano wa Baraza Kuu TUGHE Taifa uliofanyika katika Ukumbi wa EDEMA Mkoani humo. 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages