SHIRIKA
la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limekabidhi fedha jumla ya
Shilingi Milioni 80 ili kuboresha miundombinu ya elimu na afya katika
Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi na Halmashauri ya Wilaya ya
Mkuranga Mkoani Pwani.
Hii
inafanyika ikiwa ni utaratibu wa TPDC wa kuwajibikaji kwa Jamii (CSR)
katika maeneo yanayopitiwa na miundombinu ya bomba la gesi linaloanzia
Madimba Mkoani Mtwara mpaka Kinyerezi Dar es salaam.
Kiasi
cha fedha Jumla ya Shilingi Milioni 30 zimetolewa katika Shule ya
Msingi Mtoni na Njianne zote zikiwa Wilaya ya kilwa kwa lengo la
kuboresha Miundombinu ya elimu kwa kujenga Darasa na vyoo vya wanafunzi.
Mkurugenzi
wa Fedha na Utawala wa TPDC (Kulia) Bwn.George Seni, akikabidhi mfano
wa Hundi kwa Mhe.Diwani wa Kata ya Tingi Bwn Dayani Mkenda katika Shule
ya Msingi Njia nne.
Vilevile,
katika kuboresha huduma za afya vijijini, TPDC imekabidhi kiasi cha
Shilingi Milioni 50 kwa Halmashauri ya Kijiji cha Mwanambaya- Wilaya ya
Mkuranga Mkoa wa Pwani kwa ajili ya ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto
katika Zahanati ya Mwanambaya.
Akiongea
katika hafla hiyo, Bwn Seni alisema "ili kuwa na Taifa bora lenye
wananchi yenye afya na nguvu ni lazima watoto wazaliwe katika mazingira
yaliyo na huduma bora za afya, ndio maana TPDC imeona vema kujenga Wodi
ya mama na Mtoto ili kuwezesha huduma bora".
Mkurugenzi
wa Fedha na Utawala wa TPDC Bwn.George Seni (Mwenye Suti), akikabidhi
mfano wa Hundi kwa mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mkuranga Bwn.Athmani Manicho (Mhe.Diwani).
Bwn.Manicho
aliahidi kutoa ushirikiano ili kuhakikisha fedha hizo zinatumika
ipasavyo katika kujenga Wodi hiyo. Alieleza kuwa Wodi hiyo itahudumia
jumla ya vitongoji saba (7) vilivyopo katika kijiji cha Mwanambaya
vyenye wakazi zaidi ya 5,500.
Zahanati ya Mwanambaya, Mkuranga.Hapa ndipo kutajengwa Wodi ya Mama na Mtoto.
Kwa
nyakati tofauti, wanufaika wa fedha hizo walitoa shukrani za dhati kwa
*TPDC* kwa kuendelea kuboresha huduma za kijamii hasa katika Afya na
elimu.
Akiongea
katika hafla ya kukabidhi fedha za ujenzi wa darasa katika Shule ya
Msingi Njia nne,Mhe.Diwani wa kata ya Tingi Bwn.Dayani Mkenda alitoa
shukrani kwa TPDC kwa kuendelea kutatua kero mbalimbali za kijamii
ikiwemo kuboresha miundombinu ya shule ili kuwezesha wanafunzi kusoma
katika mazingira yaliyo rafiki.
"Kwa
darasa hili linalojengwa kwa fedha za TPDC litawezesha wanafunzi kukaa
vizuri darasani na kujisomea bila usumbufu" alionge Bwn. Dayani.
Sehemu ya wananchi waliohudhuria hafla ya kukabidhi fedha hizo .
#TPDCTUNAWEZESHA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇