Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Aloyce
Kamwelwe na Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania,Mizengo Pinda kwa pamoja
wakikata utepe kuasharia kuuzindua mfumo wa kidigitali utakaowezesha
ndege kutua salama katika Kiwanja cha Ndege Mpanda, Mkoani Katavi.
Afisa Muongoza Ndege Mwandamizi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania
TCAA Sunday Walinda akimpatia Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe maelezo ya kitaalamu kuhusu mfumo wa
kidigitali utakaowezesha ndege kutua salama katika Kiwanja cha Ndege
Mpanda, Mkoani Katavi.
Rubani wa Shirika la ndege la Tanzania Rubani Hamza akielezea namna
mfumo huo ulivyorahisisha hatua za utuaji ndege katika uwanja wa ndege
wa Mpanda, Katavi.
Viongozi walioketi meza kuu wakipungia ndege ya Shirika la ndege la
Tanzania kama ishara ya kuitakia safari njema ilipokuwa ikipaa kutoka
uwanja wa ndege wa Mpanda, Katavi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza Johari
akielezea mchakato mzima ukinzia na tafiti na hatimaye kubuniwa kwa
mfumo huu wa kidigitali wa kuziwezesha ndege kutua salama katika uwanja
wa ndege wa Mpanda, Katavi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Aloyce
Kamwelwe, akielezea kufurahishwa na jitihada zilizofanywa na Mamlaka ya
Usafiri wa Anga Tanzania kufanikisha mfumo huu kukamilika sambamba na
kuipongeza mamlaka hiyo kwa kutumia wataalamu wazawa waliobuni mfumo huu
katika Kiwanja cha Ndege Mpanda, Mkoani Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh Juma Zuberi Homera ameipongeza TCAA kwa kubuni
mfumo huu na kusisitiza kuwa wananchi wa Mpanda watumie fursa hii ya
ujio wa ndege mara tatu kwa wiki kujiimarisha katika kuwekeza kwani
milango ya biashara na wageni zaidi kufika mpanda kwa usafiri wa anga
sasa imerahisishwa.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Mh. Mizengo Pinda akiwachagiza
wanaMpanda kuitumia fursa hii ya ujio wa ndege katika wilaya hiyo
kujinufaisha kiuchumi.
Your Ad Spot
Dec 29, 2019
Home
featured
Usalama
TCAA WAZINDUA MFUMO WA KIDIGITALI KUSAIDIA KUTUA NDEGE KIWANJA CHA NDEGE MPANDA - KATAVI
TCAA WAZINDUA MFUMO WA KIDIGITALI KUSAIDIA KUTUA NDEGE KIWANJA CHA NDEGE MPANDA - KATAVI
Tags
featured#
Usalama#
Share This
About Richard Mwaikenda
Usalama
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇