Katibu
Mkuu- Mafunzo ya ufundi wa wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,
Avemaria Semakafu, akizungumza wakati wa kutoa tuzo na zawadi kwa
wanafunzi bora wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), jijini Dar
ea Salaam leo.
Mkuu
wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, Preksedia Ndomba akizungumza
wakati wa kutoa tuzo na zawadi kwa wanafunzi bora wa Taasisi ya
Teknolojia Dar es Salaam (DIT), jijini Dar ea Salaam leo.
Mmoja
ya wafadhili wa tuzo na zawadi, Christopher Mgonja akizungumza na
wanafunzi wakati wa kutoa tuzo na zawadi kwa wanafunzi bora wa Taasisi
ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), jijini Dar ea Salaam leo.
Mwenyekiti
ya bodi ya Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam,profes Apollinaria
akizungumza na wanafunzi wa DIT wakati wa kutoa tuzo na zawadi kwa
wanafunzi bora wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), jijini Dar
ea Salaam leo.
Katibu Mkuu- Mafunzo ya ufundi wa wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Avemaria Semakafu, akiwakabidhi tunzo Baadhi ya wanafunzi bora wa Taasisi ya DIT jijini Dar ea Salaam leo.
TAASISI
ya Teknolojia Dar es Salaam(DIT), imeaswa kuweka atamizi ya wanafunzi
wanaomaliza katika taasisi hiyo ili itokea uharibifu wa kompyuta katika
taasisi z serikali waweze kuzitengeneza na si kutafuta mafundi wengine.
Katibu
Mkuu-Elimu ya ufundi katika Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia,
Avemaria Semakafu ameyasema hayo wakati akitoa tuzo kwa wanafunzi
waliofanya vizuri katika vitivo mbalimbali katika taasisi ya Teknolojia
Dar ea Salaam (DIT) leo jijini Dar es Salaam.
Amesema kompyuta zilizopo katika vyuo vya ualimu zimekaa kama mapambo kutokana na kuharibika.
"Tunakompyuta
kibao katika vyuo vyetu vya ualimu lakini tunaambiwa sijui teknoloji
gani imekosekana inahitajika kuzitengeneza programu ili ziweze kusoma,
zimekaa kama mapambo. Kwahiyo kweli mnakuwa na atamizi hapa mtashindwa
kwenda kututengenezea kweli. Kwa hiyo ninaomba nikualike mje mtufufulie
kompyuta zile".
Avemaria amesema badala ya kwenda kutafuta fundi wa kutengeneza kompyuta mtaani, huko ni kuchezea fedha za walipa kodi.
Kwahiyo viundwe vikundi ambavyo vitasaidia kutengeneza kompyuta hizo.
"Kwahiyo mje mtusaidie kutengeneza kompyuta zetu".
Hata
hivyo Semakafu amewashauri Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),
kuweza kushiriki moja kwa moja kanyika kuhakikisha kuunga mkono kazi za
kibunifu zinazofanywa na wanafunzi wa taasisi ya Teknolojia Dar es
Salaam (DIT), ziweze kuendelezwa.
Pia
amewapongeza wanafunzi waliopata tuzo na zawadi, ni ishara ya kutambua
na kuenzi juhudi kubwa wanazozifanya katika kujifunza na kuhakikisha
wanafanya vyema katika mitihani na majaribio mbalimbali katika fani zao.
Kwa
upande wake Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Preksedis
Ndomba amesema kuwa wanafunzi wanatakiwa kupendekeza matatizo
yanayoikumba jamii yao na kuyatatua.
Ndomba
amesema kuwa taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam inataoa tuzo kwa
wanafunzi wanaofanya vizuri ili kuhamsisha juhudi na maarifa katika
kushindana katika masomo wanayofundishwa.
Hata
hivyo Mwenyekiti wa bodi ya DIT, Profesa Apollinaria amewapongeza
walimu wanaowafundisha wanafunzi hao na mpaka kupata tuzo.
Mmoja
ya wafadhidhi wa tuzo zilozotolewa na Taasisi ya Teknolojia Dar es
Salaam, Chrostopher Mgonja amesema wanaamini kuwa vijana wote ni wazuri,
na amewaomba vijana hao wakawe chachu huko wa endako na kuwafundisha
wengine ili waweze kufaulu masomo yao.
"Tunacho
waomba mkawe chachu huko mnakoenda na mjitahidi kuwatia moyo wenzenu
ambao bado wapo hapa, naamini mnaweza mkawapa ujanja naweza kufaulu kwa
namna gani".
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇