LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 21, 2019

TAARIFA KWA UMMA: MVUA KUBWA KATIKA MAENEO MENGI NCHINI. MICHUZI BLOG AT SATURDAY, DECEMBER 21, 2019 TAARIFA, Dar es Salaam, 20 Disemba 2019: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa taarifa ya uwezekano wa kutokea kwa vipindi vya mvua kubwa katika maeneo mengi nchini. Mvua zinazoendelea katika baadhi ya maeneo ya Nyanda za juu kusini magharibi pamoja na kanda ya kati zinatarajiwa kusambaa katika maeneo mengine ya nchi. Hali hii inatokana na kuimarika kwa ukanda mvua na kusogea zaidi katika maeneo hayo. Hivyo, tahadhari ya vipindi vya mvua kubwa kwa siku ya kesho tarehe 21/12/2019 inatolewa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Pwani, Dar es salaam, Tanga, Morogoro, Dodoma, Singida, Lindi, Mtwara, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Ruvuma pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba. Aidha, kwa tarehe 22/12/2019 vipindi hivyo vya mvua kubwa vinatarajiwa kupungua. Hivyo, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inatoa Angalizo la mvua kubwa. Kutokana na uwepo wa mgandamizo mdogo wa hewa kaskazini mashariki mwa Madagascar TMA inaendelea kufuatilia mwenendo wa mgandamizo huo pamoja na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa nchini. USHAURI: Wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia utabiri wa saa 24 pamoja na tahadhari kila zinapotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na kuchukua hatua. Imetolewa na; Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Mawasiliano yote yaelekezwe kwa: Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Morogoro Rd, Ubungo Plaza, Ghorofa ya 3 S.L.P. 3056, Dar es Salaam, Tanzania. Nukushi: +255 22 2460735, Simu: +255 22 2460706-8 Barua pepe: met@meteo.go.tz, Tovuti: www.meteo.go.tz (IMETHIBITISHWA – ISO 9001:2015, Huduma za Hali ya Hewa kwa Usafiri wa Anga)


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa taarifa ya uwezekano wa kutokea kwa vipindi vya mvua kubwa katika maeneo mengi nchini. Mvua zinazoendelea katika baadhi ya maeneo ya Nyanda za juu kusini magharibi pamoja na kanda ya kati zinatarajiwa kusambaa katika maeneo mengine ya nchi. Hali hii inatokana na kuimarika kwa ukanda mvua na kusogea zaidi katika maeneo hayo. 
Hivyo, tahadhari ya vipindi vya mvua kubwa kwa siku ya kesho tarehe 21/12/2019 inatolewa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Pwani, Dar es salaam, Tanga, Morogoro, Dodoma, Singida, Lindi, Mtwara, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Ruvuma pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba. 
Aidha, kwa tarehe 22/12/2019 vipindi hivyo vya mvua kubwa vinatarajiwa kupungua. Hivyo, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inatoa Angalizo la mvua kubwa. 
Kutokana na uwepo wa mgandamizo mdogo wa hewa kaskazini mashariki mwa Madagascar TMA inaendelea kufuatilia mwenendo wa mgandamizo huo pamoja na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa nchini. 
USHAURI: Wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia utabiri wa saa 24 pamoja na tahadhari kila zinapotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na kuchukua hatua.
Imetolewa na; 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. 
Mawasiliano yote yaelekezwe kwa:
Mkurugenzi MkuuMamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Morogoro Rd, Ubungo Plaza, Ghorofa ya 3
S.L.P. 3056, Dar es Salaam, Tanzania. Nukushi: +255 22 2460735, Simu: +255 22 2460706-8 Barua pepe: met@meteo.go.tz, Tovuti: www.meteo.go.tz
(IMETHIBITISHWA – ISO 9001:2015, Huduma za Hali ya Hewa kwa Usafiri wa Anga) 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages