KUTOKANA na somo la Ujasiliamali kuwa na umhimu katika kuzalisha wataalamu mbalimbali chuo kikuu cha Dar es Salaam kunafundisha somo la ujasiliamali kwa kila mwanafunzi na mwananchi anayetaka kusoma kozi hiyo.
Hayo ameyasema Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uvumbuzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dk.Ameria Buriyo wakati akizungumza na michuzi blog katika maonesho ya nne ya bidhaa za viwanda yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya J.K.Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa chuo kimeweka utaratiu mzuri kikishirikiana na shule ya biashara ya chuo kikuu cha Dar es Salaam, kwaajili ya kuhakikisha kwamba kila mwananfunzi katika chuo hicho anapata mafunzo ya ujasiliamali.
"Kwahiyo zimeshatengenezwa kozi za mwaka wakwanza kwa wanafunzi wote wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, kwa mwaka wa tatu, kwa mwaka wa nne, kwa mwaka wa tano ikiwa na maana kwamba wale wa mwaka wa mwisho". Amesema Hata hivyo Dk.Ameria
Dk.Ameria amesema kuwa kwa sasawameanza kutengeneza kozi kwaajili ya wanafunzi wa shahada za juu kwa kila mwanafunzi anayepita katika chuo kikuu cha Dar es Salaam aweze kusoma Ujasiliamali.
Hata hivyo Dk.Ameria ametoa wito kwa watu wote waliopo mitaani kuwa wameanzisha programu maalumu ya ubunifu na ujasiliamali ambayo itakuwa ikiendeshwa kila mwaka ifikapo Agosti na Septemba maalumu kwaajili ya wanaomaliza masomo yao katika vyuo vikuu vyote.
Amesema kuwa kwa mwaka huu wameshawafikia wananchi zaidi ya 2,000 katika mikoa nane ya Tannzania bara na mikoa 2 ya Zanzibar ambapo waliweza kuwafundisha somo la ubunifu na ujasiliamali.
Kwa upande wake Hezekiah Sawa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaa, amesema kuwa somo la ujasiliamli limemwezesha katika kutengeneza jiko linalotumia mionzi ya jua kupika chakula (Solar Cooker).
Amesema kuwa jiko hilo linasaidia katika utunzaji wa mazingira, utunzaji hewa pamoja na afya ya kila mtumiaji kwani halitoi moshi wa kuathiri mazingira.
Nae Mwanzilishi wa wa kifaa cha kutunzia kumbukumbu za mauzo na manunuzi(Smart Stock), Joshua Mshana na Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, amesema kuwa kifaa hicho kinamanufaa makubwa kwa mfanyabiashara mdogo na mkubwa kwaajili ya kutunza kumbukumbu za bidhaa anazouza au kununua kwa miaka mingi zaidi kuliko kuiandika kwenye daftari zinazo lowa na kuchakaa au kuungua.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uvumbuzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dk.Ameria Buriyo akizungumza na michuzi Blog jijini Dar es Salaam leo katika maonesho ya nne ya bidhaa za viwanda yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya J.K. Nyerere maarufu kama sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mbunifu kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, Joshua Mshana akizungumza na baadhi ya wananchi waliofika katika maonesho ya nne ya bidhaa za viwana yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya J.K.Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam. Joshua anaelezea kuhusiana na kifaa kinachoweza kumwezesha mfanyabiashara mdogo na wakati kuhifadhi taarifa za mauzo na manu nunuzi ya bidhaa katika biashara yake kifaa hicho chenye jina la SMART STOCK.
Mkuu wa wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva akizungumza na mmoja ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam leo mara baada ya kutemelea banda la chuo hicho leo katika maonesho ya nne ya viwanda yanayofanyika katika viwanja vya J.K.Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam leo.
Wananchi wakipata maelezo ya bidhaa malimbali zinazopatikana katika banda la chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Mwananchi akipewa maelekezo ya jiko linalotumia mionzi ya jua kupikia chakula. Katika Maelezo ya Jiko hilo linaweza kupika chakula chochote ila kwa kutegemea hali ya jua la siku hiyo.
Hata hivyo jiko hilo linatakiwa liwe juani ndipo lipike chakula kinachohitajika kwa siku hiyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇