NA TIGANYA VINCENT
MKUU
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amemwagiza Mhandisi wa ujenzi wa Ofisi
yake kuchunguza vipimo vya nyumba ya makazi ya Mkuu wa Wilaya ya Kaliua
ili kujiridhisha kama Mkandarasi amefuata maelekezo yaliyopo kwenye
ramani ya ujenzi.
Amechukua
hatua hiyo baada ya kubaini sehemu ya ukuta wa sebule katika nyumba
hiyo kurudishwa ndani mita moja na kuwa sita badala ya saba ambazo ndio
zinaoonyeshwa kwenye mchoro wa ramani ya ujenzi.
Mkuu
wa Mkoa ametoa agizo hilo Wilayani Kaliua wakati alipoongoza Kamati ya
Mkoa wa Tabora ya ukaguzi wa miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa
baada ya kupata fedha toka Serikalini.
Amesema
kama itabainika kuwa Mkandarasi amesogeza ndani ukuta kwa ajili ya
kupunguza vipimo itabidi akatwe sehemu ya fedha zake ili kufidia sehemu
ambayo imepunguzwa.
“Kwa
sababu jengo limeshafika hatua ya uezekaji , hatuwezi kumwambia abomoe
lakini tunachotaka kujua vipimo vya upana na urefu wa vyumba kama viko
sawa na kama haviko sawa kulingana na mchoro tumkate fedha” alisema.
Nyumba
hiyo ya makazi ya Mkuu wa Wilaya ya Kaliua inaendelea kujengwa na
Mkandarasi ambaye ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) inatarajia kutumia
shilingi milioni 199.6 hadi itakapokamilika.
Aidha
Mkuu huyo wa Mkoa alimwagiza Mkandarasi huyo kuhakikisha anafanyia
marekebisho eneo la ndani ya Choo katika nyumba ya Katibu Tawala wa
Wilaya ya Kaliua kabla ya kuikabidhi kwa uongozi wa Wilaya ili kuondoa
mapungufu yaliyoonekana.
Katika
hatua nyingine Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu alisema
kuwa mchakato wa awali wa ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kaliua
umeanza na tayari wameshapokea shilingi milioni 350 kwa ajili ya kuanza
kazi za awali za ujenzi wa Ofisi hiyo ambapo tayari uchunguzi udongo
umeshafanyika.
Aidha
Katibu Tawala huyo wa Mkoa alisema kuwa awali walitaka kutumia Shirika
la Nyumba la Taifa katika ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya lakini
wakadai shilingi bilioni 1.400 ikiwa ni gharama za ujenzi pekee tu bila
kuweka gharama za ununuzi wa vifaa.
Alisema
hatua hiyo iliwafanya kuachana nao na kuendelea kutafuta Wakandarasi
wengine ambao watajenga jengo hilo kwa ubora unaotakiwa kwa gharama za
chini.
Viongozi
wa Mkoa wa Tabora na Wilaya ya Kaliua wakiwa nje ya jengo la Makazi ya
Mkuu wa Wilaya ya Kaliua wakati wa ziara yao ya kukagua miradi
mbalimbali ikiwemo ujenzi huo unaoendelea.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (katikati) akitoa maelekezo kwa
Watendaji na viongozi mbalimbali mara baada ya kukagua maendeleleo ya
ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Kaliua.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kulia) akipima urefu wa kuta
mbalimbali wakati wa ukaguzi wa maendeleleo ya ujenzi wa nyumba ya Mkuu
wa Wilaya ya Kaliua.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kushoto) akitoa maelekezo kwa
Watendaji na viongozi mbalimbali mara baada ya kukagua maendeleleo ya
ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Kaliua . Picha na Tiganya Vincent
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇