Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akionesha taka zilizojaa na
kuziba sehemu ya kupita maji katika daraja la Kigogo, Dar es Salaam, wakati wa
ziara ya kukagua leo miundomnu iliyoathiriwa na mafuriko ya mvua iliyonyesha
jijni jana. Nyuma yake ni Mkuu wa Walaya ya Kinondoni, Godrey Chongolo. Makonda
amewaasa wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuacha tabia ya kutupa ovyo taka
kwenye mito. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiruka nguzo ya daraja baada
ya kukagua athari ya mafuriko eneo la Shekilango, Sinza Dar es Salaam.
Jengo la ghorofa likiwa limeathirika lwa mafuriko ya mto Ng’ombe, eneo la
Tandale Uzuri. Waliokuwa wanaishi humo tayari wote wamehama.
Mkazi wa Kigogo akielezea jinsi mafuriko yalivyoikumba nyumba yao eneo la
Kigogo Darajani.
Athari za mafuriko eneo la Daraja la Shekilango, Sinza
Baadhi ya Taka zinazotupwa ovyo na baahi ya wakazi wa Jiji zikiwa zimekwama katika daraja la Shekilango, Mto Ng.ombe na kusababisha maji kutopita kirahisi hivyo kusababisha mafuriko.
RC Makonda akiongea na maofisa wa Kampuni ya China Henan, ambapo aliwahoji kuhusu maendeleo ya ujenzi wa madaraja na kingo za mto Ng'ombe, eneo la Tandale Uzuri, Dar. Aliwahimiza kuongeza spidi ya ujenzi.
Katapila la Kampuni ya China Henan ikichimba eneo patakapojengwa daraja Tandale Uzuri, Chai Bora.
Baadhi ya wakazi wa Tandale Uziri Chai Bora, wakipita kwenye maji eneo lililoathirika kwa mafuriko
RC Makonda akiangalia eneo lililoathirika kwa mafuriko Tandale Uzuri. Kulia kwake ni Mkuwa Wilaya ya Kinondoni, Godfrey Chongolo.
Katapila la Wakala wa Taifa wa Barabara (Tanroads), likiondoa matope yaliyokuwa yamejaa barabarani eneo la Jangwani na kusababishwa barabara kufungwa kwa muda. Yaliruhusiwa mabasi ya Mwendo kasi tu.
Wakazi wa Dar es Salaam wakitembea kwa miguu eneo la Jangwani ambalo barabara ilifungwa kupisha kuondolewa kwa matope yaliyosababishwa na mafuriko.
Bai la Mwendokasi likipita Jangwani eneo ambalo matope yameshaondolewa.
Ni swaga kwa kwnda mbele baada ya Barabara ya Morogoro kufungwa eneo la Jangwani
RC Makonda akizungumza na wanahabari kuhusu hatua wanazozichukua kurekebisha miundombinu iiyoathiriwa na mafuriko.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇