LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 21, 2019

NMB YAWAZAWADIA WASHINDI WA KAMPENI YA MASTABODA SIMU NA HELMET

 Meneja Mwandamizi Idara ya Kadi NMB Bank, Manfred Kayala akimkabidhi zawadi ya simu mmoja wa washindi wa kuweka miamala 200 kupitia Mastercard QR kwa waendesha bodaboda Mastaboda, katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya benki hiyo, Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Waendesha Bodaboda na Bajaji Dar es Salaam, Michael  Massawe. Januari mwakani watatoa zawadi ya bodaboda tano aina ya boxer, ambapo mshindi wa bodaboda moja itabidi afikishe miamala  600
 Washindi wa Kampeni ya Mastaboda wakifurahia jambo baada kuambiwa kuwa  wanazawadiwa kila mmoja simu na kofia ngumu wakati hafla hiyo.
 Meneja Mwandamizi, Idara ya Kadi, Bidhaa za Kadi wa NMB Bank,Lupia Matta akielezea kuhusu mafanikio ya kampeni ya Mastaboda wakati wa hafla ya kuwazawadia washindi simu na kofia ngumu (Helmet). MastaBoda ni kampeni ambayo inalengo la kuwafikia waendesha bodaboda zaidi ya Milioni 2 nchi nzima, ila kufikia 2020 watakuwa wamewafikia elfu 75.
  Meneja Mwandamizi Idara ya Kadi NMB Bank, Manfred Kayala akimkabidhi mshindi mwingine zawadi ya simu.
 Meneja Mahusiano wa  Idara ya Kadi NMB Bank, Yusuf Adiayo akimpongeza mmoja wa washindi
 Mwendesha Bodaboda akifurahia zawadi ya simu baada ya kukabidhiwa
Mwenyekiti wa Waendesha Bodaboda na Bajaji Dar es Salaam, Michael  Massawe akimvisha kofia ngumu zawadi iliyotolewa sambamba na simu kwa washindi wa masterboda
 Ni furaha iliyoje kwa Adam Gunza  baada ya kupata zawadi ya simu na kofia ngumu
 Viongozi wa NMB Bank Idara ya Kadi, wakiwa katika picha ya pamoja na washindi.
 Meneja Mahusiano wa  Idara ya Kadi NMB Bank, Yusuf Adiayo akiwa na washindi wa kampeni ya Mastaboda

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages